ENZI ZILE-barmedas.tv

Tulikotoka: picha hiyo inaonyesha barmedas.tv ikiwa na kikosi cha kazi ilipokuwa na vijana wachapa kazi kutoka kushoto Kassim Mashaka- Camera man, Ashiraf Yusuph- Graphics, Mwl Sokoro- Programs Manager na Peter Mukajanga- Camera Man wote wakiwa ni wafanya kazi wa barmedas.tv huo ukiwa ni Mwaka  2013.

Picha hii inakumbukumbu kubwa kipindi barmedas.tv ikiwa inatoa huduma kwa njia ya Cable peke yake, ilikuwa ikionyesha vipindi mbali mbali katika Channel zake enzi hizi zilikuwa ni Channel chache kama, barmedas, Africana, 24/7 Sports , Mwanza Tv Guide ( MTG) na Mwanza Live leo barmedas imeendelea kupiga hatua na kuongeza Channel kama HeaveN, Muzika, Swahili Move na hatimae Hashikome Channel hizi kila moja inapendwa na kuwa na watazamaji wengi.

Na sasa cha kupongezwa ni baada ya Channel ya barmedas, kupandishwa kwenye Setelite hivyo kuonekana sehemu kubwa ya Nchi za Afrika lakini pia na nje ya mipaka ya Afrika na pia Channel hiyo inaonekana kwenye king'amuzi cha Star times hii, ni hatua kubwa sana .

Pia inaendelea kurusha matukio yote yanayoyo tokea katika Mkoa wa Mwanza husisani katika Jiji la Mwanza lakini pia itaanza kuwa na taarika kutioka Mikoani baada ya kuwa na Maripoter katika Mikoa mingine ambao watakuwa wana report kutoka huko na kutuma taarifa na matukio moja kwa moja barmedas.tv

Watazamaji wameongezeka sana haswa  kwa kupendezwa na vipindi vinavyooneshwa na Channel zake hakika barmedas.tv imepiga na inaendelea kupiga hatua ikiwa na Kauli yake ya " Sisi tunatangulia na wengine, wanafuata"

Comments

Popular Posts