IBADA ZETU-barmedas.tv

Mchungaji Zacayo Bugota  Katibu Mkuu wa AICT akimuweka Wakfu mtumishi wa Mungu  Mhubiri Ask wa Dioces ya Tabora na pia Ask Mkuu wa AICT Rev Silas Kezakubi.

NENO KUU: Mhubiri 2:24 Ask Kezakubi alieleza kwa kifupi kuhusu Watoto wa Yakobo, Kabila la Walawi halikupewa Urithi bali Mungu ndiye alikuwa Murithi wao.

Aliendelea kuwaelezea hawa Walawi jinsi Mungu
Alivyolichagua Taifa la Israel Kabila la Walawi Zaka ilitumika katika kuwatunza Walawi, Walawi ni Kabila la 12 huko Israel.

Alirejea kwa Wakristo kuwahimiza  Wakristo kuwatunza watumishi wa Mungu,  aliwaasa Wakristo waweze kutoa Zaka ili iwatunze Watumishi wa Mungu "Lete Zaka kamili Nyumbani mwa Bwana" Zaka ipeleke Nyumbani mwa Bwna ili hao Walawi (Watumishi wa Mungu)iwatunze nawe "Utabarikiwa"

Ask Silas Kezakubi alikuwa akiwafundisha Wakristo kuhusu utoaji, "Watu wanamdanganya Mungu kwa utoaji wa zaka na Sadaka si sahihi wanavyomutolea Mungu alivyowabariki, Askofu aliwaomba wawe na uaminifu kwa kazi hiyo ya utoaji.

Comments

Popular Posts