SIASA YA TANZANIA- barnedas.tv

Mtazamo juu ya Siasa ilipofikia sasa Tanzania, taswira yake haitabiriki kwa kuwa sasa Wanasiasa wazi wazi wanaonyesha moyo wa kutaka madaraka haswa kutawala.
Kwa nini nasema hivyo, wanasiasa wamekuwa wagombea nafasi mbali mbali hawa kipindi hiki wamekuwa wakivihama vyama vyao vya awali na kwenda kwenye vyama pinzani ukiona kinachotafutwa hapa! ni kupata nafasi ya Ubunge ama Udiwani (Madaraka).
Kama wangeliweza kugundua viongozi wa vyama mbali mbali, wasingeliweza kuwapokea na kuwapa nafasi moja kwa  moja za kugombea pasipo kuwachunguza maana wanakotoka  kwenda upande mwingine 1. Si wanachana halali, kwani hawana uchungu wala mapenzi 2.lakini pia hawana dira sahihi ya kwenda kukisaidia Chama hicho sahihi kwa kuwa wanakuwa wangali ni wageni katika chama husika , lakini kwa kuwa sasa Chama kinaangalia mtaji wa Mgeni  anaeingia na kwa kuwa lengo la Chama husika ni kuchukua Dola, basi kumekuwepo na mchezo huo pasipo kuangalia madhara yake.

Hali hii imewachanganya baadhi  wanachama na washabiki wa vyama vyao kwani wanaanza kupoteza Imani zao kwao na  pia hali hii inaenda kuzimega juhudi za wanachama hai wa vyama hivyo  pia  kuzizorotesha fikira lengwa kwani ndani ya vyama kunaanza kujitokeza nyufa ,  kuja kujiziba mda unakuwa umeyoyoma.

Mimi siamini kuwa wote wanaotoka chama kimoja kwenda Chama kingine  kufika kupewa madaraka hilo linadhihilisha ni jinsi gani upande huo haukuwa umejizatiti lakini pia hama hama hii itaenda kwenye vyama vyote, nawengine wataanza kurudi kule walikotoka hilo lipo, haswa itakapokaribia kipyenga cha upigaji wa Kura kukaribia tukumbuke Siasa hana rafiki wa kudumu tumeona kipindi hiki ,  marafiki watahitilafiana kisa ni siasa lakini baada ya zoezi zima la upigaji Kura watu watarudi kupendana na kuwa marafiki wema.

Lakini hali hii inaonyesha Siasa imekuwa inamabadiriko makubwa na  mwamko wa hali ya juu hivyo , viongozi waweze hakika kuwaasa wanachama wao wawe makini katika kuvishabikia vyama vyao kwa ustasarabu wakwepe siasa za uvunjifu wa Amani.
Tunapokwenda kupiga kupiga kura hivi karibuni tuwe makini sana kumuchagua kiongozi atakae leta maendeleo.
Mungu Bariki Tanzania, Mungu Bariki Afrika.

Comments