TCRA-barmedas.tv

Maofisa kutoka TCRA walizitembelea ofisi za barmedas zilizoko Mtaa wa Bantu tarehe 20.08.2015.
Picha hapo chini zikionesha Mkurugenzi wa Barmedas.Com Mr Mohin Barmeda,  akitoa maelezo kwa wageni hao kuhusu barmedas.tv inavyofanya kazi  yake na inavyopiga hatua katika Tasinia hiyo ya Habari.

Akieleza kuhusu Channel ya Mwanza Live iliwavutia wageni hao haswa ilipokuwa ikionyesha baadhi ya Mitaa na Barabara zilizoko Jijini Mwanza "Channel hii imekuwa ikitumiwa zaidi kutoa taarifa kwa Masaa 24 kuhusu hali ya hewa na Matumizi ya Barabara na hasa Majira ya Asubuhi na Jioni kunapotokea musongamano  mkubwa wa magari na pia kunapokuwa na matukio makubwa mjini kati channel hiyo hutoa taarifa kwa wateja wetu kuona haki halisi" Mkurugenzi huyo alimaliza maelezo yake huku akionekana Mtu mwenye kujitambua anachokifanya ni cha uhakika na chenye ushindani Mkubwa.

Wageni hao walivutiwa sana na utendaji pia jinsi barmedas.tv inavyojipanga  kutoa ushinda kwa vyombo vingine ambavyo vilianza kitambo katika Tasinia hiyo, na akiwachekesha wageni hao alipotoa Kauli mbiu ya barmedas "Sisi tunatangulia na wengine, wanafuata"

Comments

Popular Posts