KONGAMANO LA MAOMBI-barmedas.tv

Kongamano la maombi ya Amani la akima Mama lililoandaliwa na NITETEE FOUNDATION chini ya Mkurugenzi wa Asasi hiyo  isiyoya Kiserkali  mama Flora Lauwo, yaliyofanyika siku ya Jumapili  tarehe 06 September 2015 huko Yatch Club,  Kongamano hilo lilihudhuliwa na akina mama wa Madhehebu yote katika Jiji la Mwanza.

Akina Mama wajasiliamali kutoka Uganda na Kenya wakijumuika na wenzao wenyeji wa Tanzania husisan wa Mwanza kuhudhul8a Kongamano hilo.

Dr Asha Rose Migiro-Waziri  wa Katiba na Sheria
Akihutubia umati  mkubwa wa akina Mama walioitika kuhudhulia Kongamano hilo, alisisitiza kuwa akina Mama waendelee kuomba sana  Kampeni hadi kufikia uchaguzi "tumuombe sana Mungu ili aweze kuendelea kutupatia Amani ambayo ndio Tunu yetu sisi Tanzania"

Alijikita zaidi kuwakumbusha zaidi kuwa akina Mama nijeshi kubwa pia linaweza kufanya maajabu kwani "mimi nimekuwa Naibu Katibu wa Umoja wa Mataifa pia kupewa nyadhifa mbali mbali Serkalini na pia katika 3 bora za wagombea Urais nilikuwemo hivyo inaonyesha jinsi gani Mwanamke anaweza akafanya vizuri katika kulitumikia Taifa kuondoa zana za gikira potofu wanaoendelea kusema, eti Mwanamke ni kiumbe dhaifu.
Kongamano hili pia wageni mbali mbali waalikwa  wamehudhulia Kongamano hilo.

Comments

Popular Posts