KONGAMANO LA MAOMBI-barmedas.tv

Mkurugenzi wa Nitetee Foundation , Flora Lauwo akitambulishwa mbele ya umati wa akina Mama waliohudhulia Kongamano hilo la maombi , Kongamano la akina mama Kutoka Madhehebu ya Kiislam pia akina Mama kutoka Madhehebu ya Kikristo kila dhehebu kama wawakilishi waliliombea Taifa Amani ili uchaguzi umalizike kwa Amani na utulivu.

Konganano hilo la Maombi lilifanyika maeneo ya Yatch Club-Capri point Mwanza, akizungumza Mkurugenzi huyo aliwaomba akina Mama waiunge mkono Asasi hiyo kwakuwa tangia Asasi hiyo ianzishwe Mwaka 2013 imekuwa ikijishughulisha na masuala ya Elimu , Afya, Ujasilia mali na kuwafikia wahitaji kwa kuona ni namna gani Mwanamke aweze kunufaika na rasilimali ya Tanzania pia kumwezesha huyo Mwanamke kupata Elimu na matibabu bora na ndivyo ilivyo Asasi hiyo imefanya na hatimae kufanikiwa kama inavyoonekana sasa Asasi inaendelea kukua.

Asasi hii inamikakati kupitia Computor, Kilimo cha Kisasa, Elimu , Afya, na ujasilia mali kama ufugaji wa Kuku na ufugaji pia wa mifugo kama mbuzi ,Kondoo na Ng'ombe.

Comments

Popular Posts