Posts

Showing posts from May, 2018

Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa China, Xu Chen akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus wakati wa mkutano baina ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi (katikati) uliofanyika leo Alhamisi Mei 31, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Tume ya Madini Kutekeleza Majukumu Yake Kwa Maslahi ya Taifa Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma Tume ya Madini imetakiwa kuhakikisha inatekeleza kikamilifu jukumu la usimamizi, Udhibiti, Ukaguzi, Ufuatiliaji, Ukusanyaji wa taarifa na kuweka kumbukumbu kwa kusimamia sekta hiyo kwa uadilifu hali itakayosaidia Taifa kunufaika na uwepo wa rasilimali madini. Akizungumza wakati akizindua Tume hiyo Jijini Dodoma, Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa kuzinduliwa kwa Tume hiyo kunaashiria kuanza kwa ukurasa mpya katika sekta ya madini nchini kwa kuwa uamuzi huo ni mapinduzi makubwa hali itakayosaidia wananchi kunufaika na sekta hiyo. "Ni imani yangu, na pia ni imani ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na imani ya Watanzania wote kuwa mtatubadilishia simulizi za sekta ya madini kutoka kuwa za kukatisha tamaa na kuwa za matumaini, kuibadili historia ya sekta ya madini kutoka kuwa ya miguno na manunguniko na kuwa yakujivunia" Alisisitiza Mhe. Kairuki Akifafanua Mhe. Kairuki amesema kuwa, si kwamba Tume hiyo imepewa mamlaka makubwa bali pia imepewa imani kubwa kwa kuwa mamlaka makubwa yanakuja na wajibu mkubwa mikononi mwa watendaji wa Tume hiyo. Aliongeza kuwa Watanzania wana matarajio makubwa na Tume hiyo na viongozi wake kwa kuwa Serikali na wananchi wanaamini kuwa sekta hiyo sasa iko katika mikono safi na salama. Kutokana na imani hiyo Mhe. Kairuki amesema kuwa wananchi wanaamini Tume hiyo itatenda haki, kusimamia ukweli na kuzingatia maslahi ya kizazi hiki na kijacho ili viweze kunufaika na madini ambayo Mwenyezi Mungu amelijalia Taifa letu. Aidha, Mhe. Kairuki ameitaka Tume hiyo kuhakikisha inasimia kikamilifu wachimbaji wadogo kwa kuwatambua na kurasimisha shughuli zao ili sekta hiyo iwanufaishe kama ilivyo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano. Kwa upande wa vibali vya mauzo ya madini nje ya Nchi amesema kuwa ni vyema Tume ikafanya mapitio ya fomu na vibali ili kuhakikisha kuna maelezo na taarifa za kina za madini yanayosafirishwa kuhusu yalipotoka (origin),. Vile vile kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ameitaka Tume iandae mbinu na mikakati ya kudhibiti utoroshaji wa madini ili kudhibiti biashara haramu ya madini. Tume ya madini imetakiwa kuangalia uwezekano wa kuweka utaratibu wa kutoa bei elekezi za madini ya aina mbalimbali ambapo utaratibu huo utawasaidia wachimbaji wadogo na wa kati. Pia Mhe. Kairuki ameitaka Tume hiyo kuhakikisha kuwa kila anayefanya biashara ya madini ana leseni na ni leseni hai iliyolipiwa na kuhakikisha kwamba inathibiti watu au makampuni yanayomiliki leseni walizopewa kwa muda mrefu bila kuziendeleza kinyume na masharti ya leseni hizo. Kuwepo kwa utaratibu wa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kuona maendeleo ya uwekezaji katika migodi ambayo imepata leseni ni moja ya jukumu ambalo Tume hiyo inatakiwa kulitekeleza. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idrissa Kikula amesema kuwa wamepokea maelekezo yote ya Serikali na Tume hiyo iko tayari kufanya kazi kwa maslahi ya Taifa . Aliongeza kuwa Tume imejipanga kuhakikisha kuwa inatatua migogoro iliyopo katika sekta hiyo kwa kushirikisha vyama vyao vilivyopo katika maeneo yao. Tume ya Madini imeundwa ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha kuwa rasilimali za Taifa zinawanufaisha wananchi wote, Kutokana na azma hiyo Tume imepewa jukumu la kusimamia sekta ya madini na Wizara ya Madini kubaki na Masuala ya kisera.

Dkt. Mwakyembe : Atoa Rai kwa Kampuni ya Multichoice Kushirikiana na Wizara ya Elimu Katika Kukuza Elimu ya Sanaa. Na Lorietha Laurence-WHUSM, Dodoma Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa rai kwa Kampuni ya Multichoice nchini kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na vyuo vinavyotoa elimu ya sanaa ya filamu ili kuhakikisha wanabadilishana ujuzi na kuwa na miradi ya pamoja. Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo jana Jijini Dodoma wakati akizindua mradi wa kampuni hiyo utakaowapa fursa ya kujiendeleza kitaaluma vijana wenye vipaji katika tasnia ya filamu kwa kupata ufadhili wa mafunzo kwa muda wa mwaka mmoja katika chuo cha sanaa Jijini Nairobi nchini Kenya. “Napenda kuwapongeza Multichoice kwa kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanaleta maendeleo, huu ni mwanzo mzuri wa kuboresha taaluma kwa vijana ambao asilimia kubwa wamejiajiri katika sekta ya sanaa ikiwemo filamu” Dkt. Mwakyembe Aidha,Dkt. Mwakyembe amewataka vijana mabao wanakidhi vigezo kuhakikisha wanachangamkia fursa hiyo adimu ili waweze kuongeza ujuzi na hivyo kuwa chachu ya maendeleo pale wanaporudi nyumbani kwa kuwafundisha wengine ili elimu hiyo kuwafikia vijana wengi zaidi. Alizidi kufafanua kuwa ili kuwa na maudhui mazuri yenye kuvutia, yanayokwenda na wakati huku yakizingatia tamaduni za nchi yetu, ni lazima tuwe na wataalamu wetu wenyewe wa kuzalisha kazi hizo za kisanii, kuanzia waigizaji, waandika hadithi, waandaaji na wazalishaji. Naye Mkurugenzi Mtendaji Multichoice Africa - Mashariki na Magharibi, Bw. Maharage Chande ameeleza kuwa Multichoice Afrika imeanzisha Multichoice Talent Factory inayolenga kuwapa vijana wenye vipaji fursa maalum ya kupata mafunzo katika sekta ya filamu. “Kwa kuanzia tutakua na vituo vitatu vya mafunzo kimoja Afrika Magharibi, kingine Afrika Masharika na Afrika Kusini, ambapo vinatarajiwa kuanza rasmi mnamo mwezi Oktoba mwaka huu huku mchakato wa kupata wanafunzi utaanza mwezi Juni mwaka huu” Bw. Chande Adha Bw. Chande alisisitiza kuwa, katika kuhakikisha wanafanikisha zoezi hilo kwa ufanisi watashirikiana kwa karibu na wadau wa tasnia ya filamu hapa nchini katika mchakato mzima wa kuweza kuwapata vijana watakaofuzu kujiunga na mafunzo hayo.

Sekta ya Madini Yakua kwa Asilimia 17.5 kwa Mwaka 2017. Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma Sekta ya madini imekua kwa asilimia 17.5 ikilinganishwa na asilimia 11.5 ya mwaka 2016 ambapo ongezeko hilo limetokana na kuimarishwa kwa udhibiti wa biashara haramu na utoroshwaji wa madini, kuimarishwa kwa ukaguzi na usimamizi katika sehemu za uzalishaji, biashara ya madini pamoja na usafirishaji wa madini nje ya nchi. Waziri wa Madini, Mhe. Angellah Kairuki amesema hayo leo, Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019. "Ukuaji wa sekta ya madini pia kumetokana na kuongezeka kwa viwango vya mrabaha na kuanzishwa kwa ada ya ukaguzi wa madini kufuatia marekebisho ya sheria ya madini ya mwaka 2010 yaliyofanyika mwaka 2017 na kanuni zake," amesema Mhe. Angellah Kairuki. Aidha amesema, mchango wa sekta ya madini katika Pato la Taifa umeendelea kuimarika ambapo katika mwaka 2017 mchango huo ulifikia asilimoa 4.8. Kwa upande wa thamani ya mauzo ya madini nje ya nchi, mauzo yalifikia Dola za Marekani 1,810,697,000 mwaka 2017. "Ni matarajio yetu kuwa thamani ya mauzo inaendelea kuongezeka tena baada ya kukamilisha mageuzi makubwa ambayo tuliyaanzisha ikiwa ni pamoja na uongezaji thamani madini ndani ya chini," amesema Mhe. Kairuki. Waziri Kairuki amezitaja kazi zilizopangwa kutekelezwa kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 na Wizara ya Madini na Taasisi zake kuwa ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali yatokanayo na rasilimali madini, kuwaendeleza wachimbaji wadogo na wa kati wa madini pamoja na kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini. Amezitaja kazi nyingine kuwa ni kuimarisha ufuatiliaji wa ukaguzi wa usalama, afya, mazingira na uzalishaji wa madini katika migodi midogo, ya kati na mikubwa, kuendelea kuhamasisha uwekezaji katika miradi ya kimkakati ya Sekta ya Madini, kuendelea kuboresha mazingira ya kuwawezesha wananchi kufaidika na rasilimali madini, kuelimisha Umma na kuboresha mawasiliano kati ya Wizara na wadau mbalimbali kuhusu masuala ya madini. Vile vile kusimamia, kufuatilia na kuboresha sera, sheria, kanuni, mikakati na miongozo mbalimbali ili kuleta ufanisi na tija katika sekta ya madini, kuendeleza rasilimali watu na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kuwezesha Taasisi zilizo chni ya Wizara. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dunstan Kitandula amesema Serikali iangalie namna bora ya kuwezesha Wakala wa Jiolojia nchini ili iweze kufanya tafiti za madini yote nchini nakuwa na Kanzi Data ambayo itatumiwa na wawekezaji toka nje, ambapo itapunguza athari kubwa za kimazingira zinazosababishwa na watafiti kutoka nje ya nchi ambao wakimaliza tafiti zao nchi hainufaiki na tafiti zilizofanywa kwenye rasilimali zake. Wizara ya Madini imeomba kuidhinishiwa na Bunge mapendekezo ya Bajeti ya Fungu 100 la Wizara hiyo jumla ya shilingi 58,908,481,992 kwa ajili ya matumizi ya Wizara na Taasisi zake kwa mwaka wa Fedha 2018/2019.

RAIS MAGUFURI AANDAA FUTARI

Tahadhari yazidi kutolewa kuhusu ugonjwa wa Ebora Mwanza

ETG Yatoa Semina na Elimu kwa wakulima kisesa Jijini Mwanza

Polisi kitengo cha dawati la ukatili wa kijinsia watakiwa kuwa na kauli ...

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA VIONGOZI WA WABUNGE LA VIJANA BARANI AFRIKA

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA VIONGOZI WA WABUNGE LA VIJANA BARANI AFRIKA

Hospitali ya Sekou toure yapata msaada wa mashuka

Kaya masikini zanufaika na mpango wa Tasaf

Sheikh Kombo Ally Fundi Tafsiri ya Qur'an Mwezi Mtukufu PT 2

Sheikh Kombo Ally Fundi Tafsiri ya Qur'an Mwezi Mtukufu PT 1

Mwanza Iko hatarini kukubwa na Ugonjwa wa Ebora

Mwanza Iko hatarini kukubwa na Ugonjwa wa Ebora

Mwanza Wajipanga Kushika Nafasi ya Kwanza Elimu Kitaifa

Maadili ya Mtanzania MADA MAVAZI

Rais Magufuli Ziara ya Ghafla ,Ategua Kitendawili cha Mafuta Bandarini

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO. Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imetoa mafunzo kwa wasimamizi wanaohusika na shughuli za kemikali wapatao 60 wa Kanda ya Mashariki yatakayowasaidia kuzuia matatizo yanayosababishwa na uelewa mdogo wa masuala ya kemikali. Mafunzo hayo ya siku mbili yamefunguliwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma ya Vinasaba, David Elias kwa niaba ya Mkemia Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt. Fidelice Mafumiko. Mkurugenzi Elias amesema kuwa kemikali zina umuhimu katika maisha ya kila siku ya mwanadamu lakini pamoja na faida hizo, kemikali zikitumiwa vibaya zinaweza kuleta madhara makubwa kwa afya ya binadamu na mazingira. “Ili kudhibiti madhara yanayosababishwa na matumizi yasiyo salama ya kemikali mbalimbali Mamlaka imepewa jukumu la kutoa mafunzo kuhusu usimamizi na udhibiti wa kemikali kwa wasimamizi wa shughuli hizi hivyo Mamlaka imeshatoa mafunzo kwa wasimamizi 86 kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu,”alisema Elias kwa niaba ya Dkt. Mafumiko. Elias amefafanua kuwa kabla ya kuwekwa sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani, kemikali zilikuwa zikiingizwa nchini kiholela na kutumika pasipo usimamizi lakini baada ya sheria kupitishwa na kuanza kutekelezwa Mamlaka hiyo imepunguza madhara mbalimbali yanayoweza kusababishwa na matumizi ya kemikali. Amewataka wahusika wakuu wa shughuli za kemikali kuhakikisha kampuni zao zinasajiliwa na Mamlaka hiyo kabla ya kujihusisha na shughuli yoyote ya kemikali pia wasambazaji wanatikiwa kuhakikisha wanasambaza kemikali kwa wale tu wanaotambulika na mamlaka hiyo. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali, Christopher Anyango ametoa rai kwa wahusika wanaoshiriki katika mafunzo hayo kuwa ni vizuri wakihudhuria viongozi wa viwanda kuliko kuwatuma wawakilishi kwani ni rahisi kiongozi kuwalekeza maafisa walio chini yao. Aidha, ameongeza kuwa mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwa wanaofanya shughuli za kemikali hivyo wajitahidi kuhudhuria kwa wingi katika mafunzo mbalimbali yanayotolewa na mamlaka hiyo.

Waziri Mwakyembe atembelea eneo la Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Jijini Mwanza

Waziri Mwakyembe azindua Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Michezo Malya Na: Genofeva Matemu – WHUSM Tarehe: 15/05/2018 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wajumbe wa Bodi ya ushauri wa Chuo cha Michezo Malya kutumia kila aina ya ubunifu kuzigeuza changamoto zilizopo katika chuo hicho kuwa fursa ili kukipa chuo sura na nafasi yake stahiki kuwawezesha wahitimu kutambulika ndani na nje ya nchi. Rai hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Ushauri jana katika Chuo cha Michezo Malya katika Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza na kusema kuwa Chuo cha Michezo Malya ni chuo cha pekee nchini hivyo hakina budi kuzalisha wataalamu wa kutosha wa kufundisha michezo katika shule, vyuo mbalimbali na hata katika ukanda wa Afrika Mashariki. “Mwenyekiti na wajumbe wa bodi hii ni changamoto ya kwanza inayowakabili kuhakikisha kuwa taasisi hii yenye wajibu adhimu katika maendeleo ya michezo nchini mnaitangaza na kuiongezea thamani upya ili taasisi hii iweze sio tu kujulikana na watanzania bali vile vile ihudumie vijana wengi wenye ari kubwa ya kupata ujuzi katika michezo kutoka nchi mbalimbali” amesema Mhe. Mwakyembe Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Michezo Malya Mhandisi Dkt. Richard Masika amesma kuwa Bodi imedhamiria kufanya kazi kwa weledi, ubunifu uadilifu na bidii katika kushauri na kusimamia Chuo cha Michezo Malya ili kitekeleze ipasavyo maudhui na madhumuni ya kuanzishwa kwake. Aidha Mhandisi Dkt. Masika amesema kuwa Chuo cha Michezo Malya ni dhana muhimu katika michezo kwa taifa letu kwani kinahitaji kuwa na wataalamu wa michezo wanaokidhi viwango vya taifa na vya kimataifa hivyo chuo kizingatie kuwa na wakufunzi mahiri, mitaala bora na mafunzo yenye ithibati Kwa upande wake Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo ametoa rai kwa wafanyakazi wa chuo cha Malya pamoja na wanachuo kuwapa ushirikiano bodi hiyo mpya ya ushauri ili baada ya miaka michache Chuo cha Michezo Malya kiweze kuvune mafanikio chanya yatakayokidhi mahitaji ya wakufunzi wa michezo ndani na nje ya nchi. Naye Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Eng. Mtemi Msafiri amewaomba Wajumbe wa bodi kuangalia namna ambavyo watawaunganisha wataalamu wanaopatikana kutoka katika Chuo cha Michezo Malya na wadau hususani Wizara ya Elimu na Tamisemi kwani wadau wote wanaotoka katika chuo hicho nia yao ni moja ya kukuza michezo nchini.

MVUA YAKATA MAWASILIANO YA BARABARA KWA MUDA WA MASAA 8 MWANZA

Waziri Jafo Atembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo Wilaya Nyamagana

Khutba ya Ijumaa Sheikh Sululu Salum

Khutba ya Ijumaa Sheikh Nassoro Said Vipi tutaupokea mwezi wa Ramadhani

Bei Elekezi ya Pamba 2018 Yatajwa

I

Sheikh Rajabu Ahmad Mwezi wa kuacha vimada

Sheikh Amani Mauba na Mchungaji Dr Jacob Mutash wakutana ana kwa ana k...

AZORY GWANDA AKUMBUKWA NA WANAHABARI MWANZA WAKATI WAKIJADILI VIKWAZO KA...

MAKAMANDA WA POLISI KATIKA KUJENGA UWEZO WA KUUKABILI UKATILI WA KIJINSIA

Vikings Night Papii kocha & Nguza Viking - Villa Park Resort Mwanza

RAIS MAGUFULI AWATAKA WANAFUNZI SUA KUACHANA NA SIASA CHUONI

Bweni la wanafunzi 34 laungua moto waomba msaada

Mwanza yapata fursa ya kampuni za uwekezaji

Full show ya Usiku wa Baba na Mwana Papii Kocha na Nguza Vickings Mwanza

Machinga 32 Wapatiwa Vitambulisho

Rais John Pombe Magufuli Asema Kula Hela za Serikali ni Sawa na Kula Sumu

Kamishna Mtweve Katibu Tawala Mwanza Astaafu

UHAMIAJI WATOA SOMO LA KUMTAMBUA MHAMIAJI HARAMU

UHAMIAJI WATOA SOMO LA KUMTAMBUA MHAMIAJI HARAMU

RAIS MAGUFULI AKEMEA WAWEKEZAJI WANAOKWEPA KODI

Mwizi Aliyeiba kilo 20 za Mahindi na Mahindi hayo Kung'ang'ania Kichani...

Wafanyakazi Mwanza Watoa Kero Zao Sherehe za Mei Mosi

RAIS JOHN POMBE MAGUFULI ATOA ONYO LA MWISHO KUTOHAMISHWA WAFANYAKAZI B...