Posts
Viongozi Mkoa wa Iringa hamasisheni wananchi kutunza historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika – Mwakyembe Tarehe: 18/03/2018 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezi Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka viongozi wa Mkoa wa Iringa kuhamasisha wananchi wa Iringa kutunza utalii na historia ya ukombozi wa Bara la Afrika kwa kuthamini nafasi iliyopewa nchi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika. Waziri Mwakyembe ameyasema hayo jana Mkoani Iringa alipofanya ziara katika mkoa huo kukagua maeneo yaliyotumiwa na wapigania uhuru wa kusini mwa Afrika na kusema kuwa kihistoria Tanzania imepewa heshima kubwa na Umoja wa Afrika kutokana na mchango mkubwa iliyotoa wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika. “Zoezi la kuhifadhi nyaraka za kumbukumbu ya ukombozi wa bara la Afrika ni letu sote, linatusaidia waafrika kuandika upya historia yetu kutokana na kasi ya maendeleo ya kiteknolojia hivyo wajibu wetu sote kuwaandaa vijana ili wawe na uwezo wakuwezesha na kurithisha historia ya urithi wa ukombozi kwa vizazi vijavyo ndani na nje ya nchi” amesema Mhe. Mwakyembe Aidha Mhe. Mwakyembe amesema kuwa Mnara wa Lugalo walipozikwa askari wa kijerumani 300 na kiongozi wao ni moja ya ishara ya ushujaa na uzalendo ulioonyesha uimara wa watanzania kipindi cha harakati za ukombozi wa Bara la Afrika na kuahidi kuwa serikali itayalinda, kuyatunza na kuyaendeleza maeneo yote yaliyotumika katika harakati hizo ili vizazii vya Afrika vipate fursa ya kujua historia tuliyopitia wakati wa kujikomboa. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza ametoa wito kwa watanzania wote walio na habari za kihistoria kujitokeza na kuweza kutoa historia hiyo ili waweze kutenda na kutimiza wajibu woa kwa manufaa ya watanzania wote na kuijenga na kuisimamisha Tanzania kihistoria kwani historia ni jambo hai lisilokufa. Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdala amesema kuwa wilaya yake chini ya serikali ya awamu ya tano itahakikisha kuwa inarejesha misingi ya utamaduni wa mtanzania na historia nzuri iliyojengwa katika Bara la Afrika kwani Iringa inasifika kwa historia hiyo na kama kwa pamoja serikali kwa kushirikiana na wanairinga watayaendeleza maeneo yaliyotumika katika harakati za ukombozi utalii na uchumi wa mkoa wa Iringa vitakua. Picha na Genofeva Matemu – WHUSM
- Get link
- X
- Other Apps
Pix 1: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na Balozi wa China nchini Mhe. WANG KE alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika Pix 2: Mratibu wa programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi. Ingiahedi Mduma (kushoto) pamoja na wajumbe wengine kutoka Wizara ya Habari wakifuatilia majadiliano ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) na Balozi wa China nchini walipokutana kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam Pix 3: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiangalia kitabu alichopewa na balozi wa China nchini Mhe. WANG KE (kushoto) baada ya kufanya mazungumzo yanayohusu masuala ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Pix 4: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na Bolozi wa Umoja wa Ulaya (katikati) Mhe. Roeland Van de Greer alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika Pix 5: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) pamoja na Bolozi wa Umoja wa Ulaya (katikati) Mhe. Roeland Van de Greer wakiangalia moja ya historia iliyoifadhiwa ya harakati za ukombozi wa Bara la Afrika baada ya kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam Pix 6: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimuonyesha Bolozi wa Umoja wa Ulaya (wapili kushoto) Mhe. Roeland Van de Greer pikipiki zilizotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika. Kulia ni Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi. Ingiahedi Mduma Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM
- Get link
- X
- Other Apps
Rais Magufuli aweka jiwe la msingi ujenzi wa reli ya kisasa Dodoma
- Get link
- X
- Other Apps
UFISADI TAARIFA YA MKURUGENZI YAKATALIWA NA MADIWANI SENGEREMA
- Get link
- X
- Other Apps
SERA YA VIWANDA YAZIDI KUTEKELEZWA, RAIS MAGUFULI AZINDUA VIWANDA SHINYA...
- Get link
- X
- Other Apps
Mh Mwigulu Nchemba Amuagiza IGP kuwakamata wanaopanga njama za kutaka k...
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Bharti Bi. Tina Uneken-van de Vreede akiwa ameongozana na mwanasheria mkuu wa kampuni hiyo Bw. Mukesh Bhavnani pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano walipowasili kwa ajili ya kuanza rasmi kwa mazungumzo kati ya Serikali na kampuni hiyo kwa lengo la kufikia makubaliano yatayokuwa na tija kwa pande zote mbili kuhusu umiliki wa Airtel Tanzania leo Machi 12, 2018 jijini Dar es salaam at2: Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Bharti Bi. Tina Uneken-van de Vreede (kushoto) akiwa na mwanasheria mkuu wa kampuni hiyo Bw. Mukesh Bhavnani (kushoto kwa waziri) pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano (kushoto) walipowasili kwa ajili ya kuanza rasmi kwa mazungumzo kati ya Serikali na kampuni hiyo kwa lengo la kufikia makubaliano yatayokuwa na tija kwa pande zote mbili kuhusu umiliki wa Airtel Tanzania leo Machi 12, 2018 jijini Dar es salaam at3:Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akipeana mikono na mwanasheria mkuu wa kampuni ya Bharti Bw. Mukesh Bhavnani walipokutana kwa ajili ya kuanza rasmi kwa mazungumzo kati ya Serikali na kampuni hiyo kwa lengo la kufikia makubaliano yatayokuwa na tija kwa pande zote mbili kuhusu umiliki wa Airtel Tanzania leo Machi 12, 2018 jijini Dar es salaam at5 at 4 na at5: Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akiongozana na mwanasheria mkuu wa kampuni ya Bharti Bw. Mukesh Bhavnani pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Bharti Bi. Tina Uneken-van de Vreede na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano walipokutana kwa ajili ya kuanza rasmi kwa mazungumzo kati ya Serikali na kampuni hiyo kwa lengo la kufikia makubaliano yatayokuwa na tija kwa pande zote mbili kuhusu umiliki wa Airtel Tanzania leo Machi 12, 2018 jijini Dar es salaam at6 na at7: Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akiongoza ujumbe wa serikali katika mazungumzo na mwanasheria mkuu wa kampuni ya Bharti Bw. Mukesh Bhavnani pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Bi. Tina Uneken-van de Vreede na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano walipoanza rasmi mazungumzo yenye lengo la kufikia makubaliano yatayokuwa na tija kwa pande zote mbili kuhusu umiliki wa Airtel Tanzania leo Machi 12, 2018 jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU
- Get link
- X
- Other Apps
RAIS MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA UYOVU BWANGA NA ISAKA USHIROMBO
- Get link
- X
- Other Apps
ATHARI MAGONJWA YA FIGO,WANAWAKE WAONGOZA KWA IDADI YA VIFO DUNIANI
- Get link
- X
- Other Apps
Vijana 4 waliouwawa na wananchi wakidhaniwa ni wezi wakumbukwa
- Get link
- X
- Other Apps


