KARIBU MWANZA LIVE PROGRAM-barmedas.tv
KARIBU MWANZA LIVE PROGRAM-barmedas.tv
Mwanza Community Bank Mr Kahungwa na wageni wengine watakuwa katika kipinfi Cha Karibu Mwanza itakuwa ni murejesho wa mazungumzo ya awali ambapo pia walikuwa wageni kwenye kipindi hiki,ilionyesha kuwa watu walikuwa na shauku kubwa ya kutaka
kujua Bank hii itawanufaisha vipi wakazi wa Kanda ya ziwa na hususan wale watakao kuwa wanachama, ndizo changamoto ambazo watu siku ya kipindi hicho walipiga simu kwa wingi kutaka kujua hatima yake,
Kipindi hicho kitaambatana na zawadi kwa wale watakaojibu maswali kwa usahihi,
Joseph Kahungwa akiongea na mmoja wa watangazaji wa hapo barmedas.tv alikuwa akiyasemea mafanikio aliyoyapata baada ya kupata nafasi kuingia kafika kipindi cha Karibu Mwanza awali nikuwa watu wengi wamekuwa wakiongezeka kujiunga haswa siku za kikomo za kuchukua hisa kukaribia kuisha ambapo tarehe 30 .10.2013 ndio utakuwa mwisho wa wakujiunga na Bank hiyo kwa wana hisa.
Akisisitiza Kahungwa alipoulizwa kuwa katika kipindi cha leo tarehe 23.10.2013 atakuwa na yapi yakuwaeleza watazamaji pia
wanachama kwa ujumla? "alisema"kwanza nitachukua nafasi hiyo kuwashukuru wote waliothubutu kutuunga mkono kwa kujiunga na Bank hiyo ya wakazi haswa wa Kanda ya ziwa kujiunga kwa wingi hadi kukaribia kufikia malengo yaliyokusudiwa , mashariti waliyopewa na Bank kuu kuwa na wanahisa wengi lakini kunakiasi cha fedha ambazo lazima wazifikie ili kupewa leseni ya kuendesha Bank hiyo." Matarajio. yake Kahungwa ni kuwa, watu wataendelea kujiunga kwawingi.
Wito wake Kahungwa nikuwa wakazi wa Kanda hii ya ziwa wachangamkie fursa hii ili watu wanufaike na Bank hii,alimaliza.
Usikose kutazama kipindi hiki na wzkaxi wa Dar na Arusha pia mutaweza kukitazama kipindi hiki lakini pia kwenye mtandao jwa kutumia www.barmedas.tv wenye simu Snartphone,Desktop,Laptop,ip na zingine nyingi unaweza kukitazama kwa njia ya Online,ukiwa ofisini,safarini
Comments
Post a Comment