KIPARA IMARA-barmedas.tv

KIPAIMARA  IMARA.
Kipaimara ni kitendo cha kijana ambaye  tayari alikuwa amebatizwa akiwa mtoto
hivyo huchukua mafunzo kwa ajili ya kujifunza Biblia na kanuni zote za dini husika
Makanisa mengine huwa wanaita KATEKISIMU, kwa makanisa mengine tendo hili la kusoma KATEKEZIMU hufanyika kabla ya ubatizo wa maji mengi huanza kujifunza ndipo hujaribiwa kama ameelewa vyema mafunzo ndipo hubatizwa.

Lakini Makanisa mengine hubatiza kwanza watoto wakiwa wadogo baadae wakikua hujifunza neno la Mungu kwa Mwaka mzima hatimae huarikiwa kwa kuwekewa mikono na Askofu wa kanisa husika, natendo hili huwa la furaha kubwa kwani humfanya mhusika kuingizwa kundini na kuwa Muumini kamali ambapo atashiriki meza ya Bwana, anaweza kugombea uongozi Kanisani, anapaqta haki zote.
Makanisa haya ni kama  Roman  Catholic, Lutheran Church, Anglican na mengine yaliyoko kwenye mfumo huu.

Tendo hili la ubarikio hufanyika mara moja kila Mwaka.  Picha hizi zinaonyesha watoto eako mbele wamevaa nguo nadhifu kabisa wakipewa kiapo kutoka kwa mkuu wa Kanisa  nae ni Askofu, Ghafla hii ilifanyika katika Kanisa la KKKT USHARIKA WA IMANI- Mwanza.

Comments