MIKUTANO YA WANASIASA-barmedas.tv
MIKUTANO YA WANASIASA.
Mikutano ya wanasiasa huwa ni mhimu sana hasa kwa kipindi hiki kuwaweka sawa na kuwahabarika habari na sera za vyama vyao.
Vyama vya siasa kazi kubwa wakati kama huu, nikufanya mikutano ya hadhara na kuweza kuwapa mitazamo ya vyama vyao kuambatana pia na sera zao kuwakumbusha hii, hukifanya chama chochote kuendelea kuwa na mshikamano na umoja pia na vyama vinapokuwa na mshikamano Amani katika Nchi hupatikana.
Chama kinapowakusanya wanachama wake hai na wasiohai pia na wanavyama wa vyama vingine wanapovutika kusogea kusikiliza japo kwa saa moja mazungumzo hayo hata kama atayapuuzia msikilizaji na kuondoka atakuwa amepata kitu kitakachokuwa kikijenga hisia fulani katika Kichwa chake.
CHAMA KUIMALIKA.
Huwezi kujenga chama madhubuti kama Chama hicho, hakipati mara kwa mara mikutano kutoka kwa viongozi wao wakiwakumbusha na kuwatuliza wawe na subira kwa kila jambo, wasemaJi wa chama husika wawe wanakifahamu bara bara chama pia wawe na uzoefu mkubwa hata wa kuzibu hoja kutoka kwa vyama vingine kama kulisikika chama fulani kikisema chama kingine, huwa ni wakati mwafaka katika mikutano kama hiyo kujibu hoja toka upande wa pili pia kukanusha kwa hoja pasipo kuleta machafuko kama kuna tuhuma ama jambo ambalo ni lauzushi linaloweza kupelekea kumenya chama husika ni mhimu kukanusha na kuwaweka sawa wanachama sake lakini pasipo matukano wala majigambo.
Mikutano ya vyama inatakiwa iwe niya kujijenga chama si kuingilia kuwasema vyama vingine mkutano mzima , hapo huwafanya wanachama na wahudhuliaji wa Mkutano huo kuwa na maswali , pia kusababisha waanze kukijajadiri chama hicho na kukiona kama ni puuzi hivyo nikuwa makini sana katika kuendesha mikufano ya badhara.
Kifupi vyama vya Siasa sasa ni wakati wa kukaa na wanachama wao kuweza kuwaweka kuwa na umoja pia kuwapa mtazamo wa chama chao kwa ujumla lakini pia kuwa nanafasi chache za kuwapa , wanaweza kuuliza maswali makuu na pia viongozi wajitahidi kuyajibu kwa ufasaha pia , kuwapa vielelezo lkn majibu yawe ya matumaini na si ya kujiamini sana la yawe ya kuwajenga sana chama wake.
MIKUTANO YA HADHARA YA WANASIASA, INAVIJENGA VYAMA VYAO.


Comments
Post a Comment