USALAMA BARA BARANI - barmedas.tv
Kituo cha utangazaji cha barmedas.tv kikifanya kazi sambamba na Kikosi cha Usalama Barabarani
kuhakikisha Jiji la Mwanza linatekeleza sheria za usalama barabarani.
Picha hizo zinaonyesha Utendaji wa Kazi ufanyavyo na Jeshi la Polisi kuhakikisha usalama barabarani kwa watu wote unazingatiwa, kwa kupatab mawazo kutoka pia kwa raia ambao walitoa maoni nini kifanyike ili kuhakikishe watu wanazitumia bara bara kwa uangalifu na kufuatab sheria, mkakati ulioanzishwa sasa na Mkuu wa kikosi cha Polisi Usalama Barabarani Mkoa wa Mwaza Afande Nuru Suleimani pia wakishirikiana na kuuo cha utangazaji cha barmeadas.
Wakiongea wananchi walikuwa wakitupiana lawama kuwa waendeshaji wa vyombo vya moto huwa hawaheshimu kabisa waendaji kwa miguu ajali nyingi zinasababishwa na madreva kufanya uzembe kwa kuwadharau hawa na kuwaona kanakwmba hawana haki kwa utumiaji wa barabara.
Lakini pia waendeshaji wa Vyombo vya moto wakiwemo watu wa dala dala na boda boda pia wao walikanusha kuwa vyanzo vingi vya ajali vinasababishwa na waenda kwa mguu, maana watumiapo Bara bara huwa sio waangalifu ikiwemo kuvukas Njia pasipo kuangalia pande zote kama kunausalama, lakini pia
kwenye sehemu za Zebra hawazingatii kanuni katika uvukaji wa eneo hilo hivyo, husababisha mawasiliano kati ya abiria wanao hitaji kuvuka na madereva kutegeana na hivyo hutokea wakati mwingine ajali zisizo za lazima ( za kizembe) na kusababisha madhara makubwa .
Hivyo Kikosi hicho cha usalama bara barani kikiongozwa na Mkuu wa kikosi wameanza kampeni hiyo ambayo itakuwa ni ya kudumu.
Comments
Post a Comment