ISLAMIC YATIMA FOUNDATION-barmedas.tv
Picha hapo juu Mwl Sokoro akipokewa na wenyeji wake baadhi ya Walimu na kusalimiana mara baada ya kufika katika kituo hicho kinacholea watoto yatima, barmedas.tv walikitembelea kituo hicho na kukikuta kinafanya shughuli ya kuelimisha kama zilivyo shule zingine.
Ziara hiyo ilijumuisha na kutembelea shughuli mbali mbali zinazofanywa na kituo hicho ambacho kwa kweli Mwl Sokoro na Ujumbe wake walifurahishwa sana , ujumbe ulichukua maamuzi ya kumweleza Mwalimu Mkuu wa shule hiyo kuwa , shule hiyo inahitajika itangazwe ili wahitaji waje katika kituo hicho kupata Elimu.
Mazingira ya shule hiyo ni mazuri na Elimu itolewayo hapo ni yakiwango kizuri, Mwalimu Mkuu alikuwa akiwaeleza wageni waliomfikia hapo, naalipata nafasi ya kuwatembeza wageni wake maeneo yote ya shule ikiwa na kufika ndani ya baadhi ya madarasa na kukuta wanafunzi wakipata Elimu.
Comments
Post a Comment