NYANZA SHULE YA MSINGI-barmedas.tv
MKURUGENZI WA Barmedas.Com Mr Hirnoy Barmeda akionekana kuwa na Walimu wa Nyanza Shule ya Msingi, alipotembelea na kujionea maendeleo ya shule hiyo kongwe hapa Jijini Mwanza na
Mkoa wa Mwanza kwa ujumla, Mkurugenzi huyo ambaye amewahi kuwa mwanafunzi katika shule hiyo. akizungumza katika ziara hiyo, Mkurugenzi huyo alisema kuwa kuguswa sana na ziara hiyo kwani mengi anayakumbuka alipokuwa akisoma hapo na Kaka yake ambaye pia ni Mkurugenzi wa barmedas,tv Mr Mohin Barmeda nae alisoma katika shule hiyo ya Nyanza.
ziara hiyo ilipelekea kujua mahitaji ya shule na aliahidi kutekeleza hatua kwa hatua na kweli aliweza kutimiza ahadi zake kwa kuzifanyia kazi kero zilizokuwepo karika shule hiyo, kama kukirudisha kisima kilichokuwa kimeharibika, kulipa Bili ya umeme ambayo deni hilo lilipelekea kukatiwa Umeme, pia maji nayo yalikuwa yakidaiwa Mkurugenzi alimaliza kero hizo, kwa kuwashirikisha pia wadau wake.
Picha hapo chini zikionyesha ziara ya Mkurugenzi huyo pia akiwa na Walimu wa Shule hiyo wakiwemo Walimu Wakuu wa shule hiyo ambayo imegawanyika katika tawala na kuwa Walimu wakuu 3.






Comments
Post a Comment