BI ANGELINA MABULA-barmedas.tv

ENDAPO WANANCHI WA ILEMELA WATANICHAGUA "NITAWAFANYIA MAKUU"
Bi Angelina Silivester Lubala Mabula, aahidi Makubwa endapo Wananchi wa Jimbo la Ilemela watamchagia kuwa mbunge wao wa Jimbo la Ilemela.

Akiongea kwa ufasaha pia  akijivunia kuwa na Historia ya Wilaya ya Ilemela akiwa kama mzawa wa Wilaya hiyo alisema" mimi ninasema kuwa changamoto zilizopo katika Wilaya ya Ilemela nitahakikisha nazipunguza kama si kuzimaliza kabisa endapo nitapata  ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Mwakilishi wao Bungeni " Mimi napenda sana kufanya kazi na jamii ndio maana niliona kuacha kazi ya Ukuu wa Wilaya na kugombea Ubunge ili kuwa Karibu zaidi na Jamii tofauti nilipo kuwa Dc nilihusika zaidi na mambo ya utawala hivyo sikupata mda zaidi kushughulika na Jamii.

Hayo aliyasema alipokuwa akizungumza kupitia kipindi cha Karibu Mwanza kipindi ambacho hurushwa na kituo cha barmedas.tv , alipoulizwa na mtangazaji wa kipindi hicho Charles Sokoro kuhusu Vijana atawafanyia nini haswa sasa kunakilio cha ukosefu wa ajira?  alisema, atahakikisha ananawatafutia fursa ambazo zitawafanye wasipoteze mda vijana kama wafanyavyo sasa bali , watajikita na shughuli mbali mbali za kuzalisha mali  ambapo atawashawishi waweze kujiunga katika vikundi  waweze kupatiwa mikopo ambayo itawawezesha kufanikiwa katika maisha yao  ila aliwaonya Vijana kupoteza mda kuilalamikia Serikali kuwa haijawafanyia chochote tangia Uhuru hii ni kufuru ya hali ya juu" alionekana kuwa hapendezwi kabisa na Watu wanaobeza kuwa Serikali haijafanya lolote kuhusiana na maendeleo kwa ujumla.

Alipo ulizwa kuwa Wananchi wa Ilemela wategemee nini endapo utafanikiwa  kuwa Mbunge? " Nitahakikisha kuwa hata wao watajivunia kunichagua kwani kila jambo nitalifanya kwa mpangilio   kama ifuatayo, mipango ya mda mfupi, ya kati na mipango endelevu hasa kuwafanikisha akina Mama ambao wakiwezeshwa wanaweza kupunguza tabia iliyopo sasa  ya kulialia hawana mitaji nimuhimu kuwapa elimu ya ujasilia mali hatimae kuwapa mikopo ambayo itawafanya wapige hatua kiuchumi atahakikisha hatutawasunbua kuwakamatia vitu vyao kwani tutakuwa tumewatengea sehemu rafiki na salama zaidi.

Comments

Popular Posts