AMANI YA TANZANIA-barmedas.tv
FURAHA TANZANIA IENDELEE KUDUMU.
Picha hizo zinaonyesha furaha na Amani tele
Hiyo ndiyo haki ya Mtanzania na ni wajibu wa wa Mtanzania.
Hatupendi kabisa watanzania vurugu bali wanahitaji kabisa kila mtanzania kuwa na nyuso za furaha, Amani na Upendo ,tangia uhuru Nchi yetu tumekuwa na mshikamano wa haki ya juu hatujawahi na tusingelipenda kuwa na uso wa huzuni.
Tanzania imekuwa Nchi ya kuhamasisha na kusimamia Nchi zilizokuwa Chini ya Mkoloni zote ximejikomboa kutoka katika juhudi na mipango dhabiti ya Nchi ya Tanzania.
Tumekuwa na Nyuso za furaha na hatujutii kuwa na hali hiyo bali, tunamushukuru Mungu sana kuendelea kutupa Amani tele na utulivu.
Haitapendeza hata kidogo kuipoteza Amani hii kwa Wanasiasa kutokuridhika waweze kutupeleka maghaibuni kisa eti, kunabaadhi ya watu kwa masilahi yao Taifa zima lifanywe kuwa kimbizi katika Nchi yao hili, tulipinge kwa nguvu zote.
Sasa wakati unawadia wakati wakuwachagua viongozi ambao Mungu amekwisha wapa kibali cha kuweza kujichagulia kiongozi wamutakae ambae atawapeleka kuke tunakohitaji tuelekee na tufike.
Wito wangu , Ndg zangu tuangalieni sura za hao watanzaia wanafuraha hivyo tuendelee na sura kama hizo, Wajibu wako Ndugu yako ni kutanguliza upendo na huruma bila kusahau uaminifu katika upigaji wa kura na matokeo kuyaamini pasipo kutiliana shaka.
"MUNGU IBARIKI TANZANIA"


Comments
Post a Comment