HARAKATI ZA UCHAGUZI-barmedas.tv

Tangu zilipoanza harakati za Kujiandikisha, kuanza kwa Kampeni hadi uchaguzi  tunapoukaribia hakika , barmedas.tv  tumeshiriki kikamilifu na tunahakikisha tutaendelea  kuwahabarisha watazamaji wetu taarifa na habari moto moto na kwa haraka zaidi haswa tunapoingia katika hatua ya mwisho ya kupiga kura hatimae kumpata kiongozi atakae ipeperusha Bendela ya Tanzania  pia kuwa Amri jeshi mkuu wa majeshi yetu ya Tanzania.

Kituo cha barmedas.tv kilifika kila  maeneo palipohitajika kuwapa watazamaji wetu matukio na habari moto moto,   pia tulipata mda wa kuwahoji wagombea kwa nyakati tofauti tofauti hii, ilitufanya watazamaji wetu kutuamini kuwa hatukuwa na upendeleo  katika kipindi chote hiki na  vyama vyote kuvishirikisha katika Kampeni  zao za kujinadi kupitia kituo chetu cha barmedas.tv.

Tumefika kwenye mikutano yao yao ya Kampeni kwa kuchukua matukio na pasipo kuchelewesha tuliweza kuyarusha watazamaji ambao ndio walengwa waliweza kuyaangalia, hatukuweza kuzichakachua taarifa bali zilikuwa kama zilivyo  tukihakikisha hazina upendeleo wala uzushi wa kuleta chuki katika Jamii hilo , tunamushukuru Mungu tumekuwa waangalifu sana katika utoaji wa habari na taarifa  kwa Jamii pasipo mawaa.

Tumekutana na kuongea na viongozi wa vyama mbali mbali, watu wanaolinda usalama, wasomi mbali mbali, makada wa vyama , wabunge ambao wabania nafasi za Ubunge   pia Watu wakawaida wapiga kura na wasiokuwa wapiga kura wote hao tuliwasikiliza wanasema nini kwa Wananchi lakini pia kwa viongozi! yote hayo tulihakikisha taarifa tunazifikisha  haraka kwa  walengwa ili kupata  matukio halisi pasipo kupotosha hilo tumelifanya kwa weredi wa hali ya juu.

Comments

Popular Posts