BARAZA LA WATOTO-barmedas.tv

Mwl Sokoro kwa niaba ya Uongozi wa barmedas.tv ,  akipokea mabango kutoka kwa Mwenyekiti wa Shirika la Watoto lililoko hapa Mwanza Ndg Shaban Ramadhan alipofika katika ofisi za barmedas zilizoko Mtaa wa Bantu na kutoa zawadi hizo ambazo zitatumika katika shughuli mbali mbali katika vipindi vya Baraza la Watoto ambapo kipindi  hicho hurushwa  na kituo cha utangazaji  cha barmedas.tv.

Msaada huo pia umewahusisha UNICEF kwani ndio wafadhili wa Shirika hilo laa Watoto ambapo hupewa vitendea kazi na vitu mbali mbali kwa sababu vijana wanapata mafunzo ya utangazaji na uandikaji wa Habari.

Kituo cha barmedas. tv, kimekuwa msaada mkubwa kwa watoto hawa kwani  wamepewwa kipindi ambacho hurushwa Live bure kila sikku ya Jumamosi kwani ambapo watoto hupata nafasi ya kuongelea masuala yao katika kipindi hicho cha BARAZA LA WATOTO.

Baadhi ya watoto wamepiga hatua na kuwa watangazaji wazuri jutokana na nafunzo wanayoyapata/waliyoyapata kupitia kituo hiki.

Na kukaunda kipindi cha Kijana wa Afrika  kupitia kituo hiki ambapo kijana aliye kuwa na umri zaidi ya miaka 18 huhamia kwenye kipindi hicho  barmedas.tv imekitoa bure kwa ajili ya kuelimisha jamii hasa kupitia vijana hao.

Comments

Popular Posts