BARAZA LA MADIWANI-barmedas.tv
Mwanza
Baraza la
madiwani halmashauri ya jiji la Mwanza
limepitisha bajeti ya kiasi cha shilingi billion 87. 194 kwa mwaka wa fedha 2016/2017
ikiwa ni ongezeko la asilimia 52 ya bajeti ya mwaka ulipo 2015/2016
Mwaka wa
fedha unaoendelea hadi sasa 2015/2016 halmashauri ya jiji la Mwanza ilikuwa na
bajeti ya shilingi billion 57.307 ambapo hadi kufikia mwezi December mwaka 2015
halmashauri imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi billion 28.357 sawa na
asilimia 49.
Kupitia
bajeti hii mpya halmashauri itaongeza mapato yake kwa asilimia 62 kutoka
shilingi bilioni 11.409 mwaka uliopo hadi shillingi bilioni 15.061 kwa mpya .
Akiwasilisha
Bajeti hiyo katika kikao maalumu cha baraza hilo kilichofanyika katika ukumbi
wa halmashauri ya jiji la Mwanza kikiongozwa na mstahiki meya wa jiji la Mwanza
bwana James Bwire, mchumi wa jiji Joseph Kashushura amesema katika bajeti ya mwaka huu asilimia 60 ya
bajeti itapelekwa kwenye miradi ya maendeleo
Mbunge
Nyamagana bwn. Stanislaus Mabula
amesisitiza kuipa kipaumbele miradi ambayo ilianza kutekelezwa katika bajeti
iliyopo na haijakamilika ili kuikamilisha kupitia bajeti mpya ya mwaka
2016/2017.
Aidha
madiwani wametumia fursa hiyo kumpongeza mkurugenzi wa jiji bwana Adam
Mgoyi na Mbunge wa Nyamagana kwa kazi
kubwa za maendeleo za jiji walizozifanya mwaka wa bajeti ambao unaelekea
ukingoni.
Comments
Post a Comment