ATHANAS MDAM- barmedas.tv

ATHANAS  MDAM  ANG'ARA   NDFA.

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa "Taifa Star" Athanas Mdam ameng'ara katika ligi Wilaya ya Nyamagana
(NDFA) baada ya kuibuka kuwa mfungaji Bora wa Ligi akitokea timu ya  Alliance ya Jiji la Mwanza.

Athanas amemaliza ligi akiwa ameweka kimyani magoli jumla 21 na huku timu yake, ikiutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa point   17.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa, amefanikiwa kupachika mabao kila mechi aliyoicheza licha ya kuzikosa mechi baadhi kwa kuwajibika katika timu ya Taifa.

Ligi hiyo imekamilika, kwa ubingwa kubebwa na  Alliance, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Marsh Athletics na Kilimo Fc kumaliza ikiwa imejitwalia nafasi ya tatu ,   ligi hiyo  ikidhaminiwa na Barmedas.Com na michezo yote ikiratibiwa na barmedas.tv

Comments