Posts

Showing posts from March, 2018

Waziri Mwakyembe:Nendeni Mkashindane kwa bidii mrudi na Medali Na Anitha Jonas – WHUSM 28/03/2018 Dar es Salaam PiX 1: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa suti) akimkabidhi bendera Kapteni wa Timu ya Taifa ya Tenisi Bw.Masoud Mtalaso leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya timu zote za michezo zinazoondoka nchini kesho jioni kwenda katika mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayofanyika nchini Australia katika mji wa Gold Coast. Pix 2:Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wanamichezo wanaokwenda katika mshindano ya Jumuiya ya Madola nchini Australia na kuwataka wawe wazalendo na kutangaza utalii wa nchi leo jijini Dar es Salaam kabla ya kuwakabidhi bendera ya Taifa. Pix 3: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kamati ya Olimpiki nchini pamoja na wachezaji wanaokwenda katika mashindano ya Jumuiya ya Madola katika sherehe ya kukabidhi bendera kwa wanamichezo hao iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam,wa kwanza kushoto ni Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Bw.Rashid Gullam na wapili kulia ni Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Bw.Filbert Bayi.

Watendaji wanaosimamia Sekta ya sanaa na Taasisi kutaneni na wasanii kuelimisha taratibu na sheria zilizopo katika sekta ya sanaa - Mwakyembe Na: Genofeva Matemu - WHUSM Watendaji wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo katika sekta ya Sanaa pamoja na Taasisi zake ikiwemo BASATA, Bodi ya Filamu na TCRA wametakiwa kukutana na makundi ya wasanii wa mziki nchini kwa lengo la kuelimisha taratibu za kuwasiliana na mamlaka husika za sanaa ili zijiridhishe na maudhui ya kazi za sanaa kabla ya kuzisambaza. Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kufanya kikao na msani wa muziki wa bongo fleva Nassibu Abdul (Diamond) kujadili namna ya kuboresha maadili katika kazi za sanaa na baadaye kukutana na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam. Mhe. Mwakyembe amesema kuwa maamuzi ya kuzifungia baadhi ya nyimbo yamefanywa kwa mujibu wa sheria na si kwa utashi binafsi wa kiongozi wa wizara, hivyo wasanii na jamii kwa pamoja waelewe kwamba hatua zilizochukuliwa na Naibu Waziri Shonza hivi karibuni zilikuwa za Wizara kwa mujibu wa sheria za nchi. “Serikali haina ugomvi wowote na wanasanaa nchini bali ina tatizo na mmomonyoko wa maadili ya kitanzania nchini na kwamba kila mwanasanaa ana wajibu wa kulinda maadili ambayo ni sehemu ya utamaduni wetu” amesema Mhe. Mwakyembe Kwa upande wake Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amewasisitizia wanasanaa kufuata taratibu za kuwasilisha kazi zao za sanaa mapema kwenye mamlaka husika ili kuepusha matatizo baadaye kwani suala la kulinda maadili ni endelevu. “Wakati umefika sasa kwa Bodi ya Filamu Tanzania na TCRA kukamilisha zoezi la kuoanisha kanuni za madaraja ya kazi za sanaa ili kazi zinazofaa kuonekana na watu wazima peke yake zianze kuangaliwa saa sita usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi” amesema Mhe. Shonza Naye msanii wa muziki wa Bongo Fleva Nassibu Abdul (Diamond) ameahidi kushirikiana kwa karibu na Naibu Waziri Shonza na uongozi mzima wa Wizara ya Habari katika kusimamia maadili ya kazi za sanaa na kuwa mfano bora wa wasanii nchini katika kulinda utamaduni wa mtanzania.

Wanaotumia Mitandao ya Kijamii Vibaya Kusakwa

RAIS MAGUFULI AWATAKA WAKULIMA KUTUMIA MBOLEA INAYOZALISHWA TANZANIA

Rais Magufuli Azindua Magari 181 ya MSD, Akerwa na Ukosefu wa Viwanda vy...

Rais Dkt Magufuli azinduzi wa magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) jijini Dar es salaam leo m2: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua ghala ya dawa kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018. Pamoja naye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund Bw. Linden Morrison na viongozi wengine. m4: Sehemu ya magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) yaliyozinduliwa jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018. m15: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund Bw. Linden Morrison wakati akijaribu moja ya magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) aliyozindua jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018. m17: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua sehemu ya magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) aliyozindua jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018.Pamoja naye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund Bw. Linden Morrison na viongozi wengine. m21: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018. m23: Sehemu ya wafanyakazi wa MSD wakimshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wakati akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018. m24: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund Bw. Linden Morrison wakati akijaribu moja ya magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) aliyozindua jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018. m25: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018. Pamoja naye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund Bw. Linden Morrison na viongozi wengine. m26: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund Bw. Linden Morrison akijaribu moja ya magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) aliyozindua jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018. m27: PALE WAPIGA PICHA WANAPOPIGWA PICHA - Wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari wakiupiga picha msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund Bw. Linden Morrison (chini kushoto) na viongozi wengine wakati wakielekea kukagua magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) aliyozindua jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018. Picha na IKULU

RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI YA MATAWI KANISA LA MTAKATIFU PETRO OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM

Kifo cha Mwalimu Mponda wa TaSUBa cha igusa Serikali Na Anitha Jonas – WHUSM 22/03/2018 Dar es Salaam. Serikali imetoa pole kwa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo kwa kumpoteza Mwalimu mahiri John Mponda aliyekuwa balozi wa tasnia ya Sanaa nchini. Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza katika ibada ya kumuaga marehemu huyo iliyofanyika katika Chuo cha TaSUBa Wilayani Bagamoyo kwa ajili ya kumuaga kwani anatarajiwa kuzikwa kijiji cha Mbalizi Mkoani Mbeya. “Tunatambua mchango wa Mwalimu John Mponda katika tansia ya sanaa nchini na kupitia wanafunzi waliyopita katika mikono yake pamoja na vikundi vya vijana alivyovianzisha ambavyo amekuwa akivifundisha kazi za sanaa, hakika tumempoteza mtu makini,”alisema Mhe.Shonza. Akiendelea kuzungumza katika msiba huo Mheshimiwa Shonza aliwasihi wasanii waliyopata mafunzo kutoka kwa mwalimu huyo kuwa mabalozi kwa wasanii wenzao na kuwashauri misingi iliyobora katika katika kukuza na kuendeleza kazi za sanaa. Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha TaSUBa Dkt.Herbert Makoye alisema kuwa marehemu mwalimu Mponda ameondoka katika kipindi walichokuwa wanamuhitaji sana kwani kwasasa taasisi hiyo ipo katika maandalizi ya Tamasha la Utamaduni la Bagamoyo ambalo nilakimataifa na hufanyika kila mwaka na yeye alikuwa mratibu na mpaka mauti yanamfika alikuwa akiwa shughulikia maandalizi hayo. “Kwa hakika msiba huu ni pigo kwa taasisi yetu na mwalimu huyu alikuwa kiungo miongoni mwetu na alifanya kazi yake kwa weledi na kujituma alikuwa ni mtu aliyeipenda kazi yake ,’’alisema Dkt.Makoye. Pamoja na hayo nae Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi waliyosoma TaSUBa Deosonga Njelekela alisema kuwa mwalimu huyo kwao hakuwa tu kama mwalimu bali alikuwa baba na mlezi kwani na alikuwa mstari wa mbele kutoa nasaha zake kwa lengo la kutaka wanafunzi wake waweze kufanikiwa zaidi. Hata hivyo nae mtoto wa Marehemu Bi. Mery Mponda aliwashukuru watu wote waliyojitokeza kuungana nao katika msiba huo kwa imekuwa ni faraja kubwa kuona watu wakiomboleza pamoja nao baada ya kumpoteza baba yao mzazi ambaye alikuwa mlezi na nguzo ya familia.

IGP Mstaafu Ernest Mangu Apelekwa Rwanda kuwa Balozi

DC Nyamagana Atoa mwezi Mmoja kwa Tax Bubu, Bajaj na Gari Ndogo za Mizig...

Taharuki Mbinu Chafu ya Ufungaji Cheni Magari Mjini

Jeshi la Zimamoto Mwanza Laendeleza Mafunzo kwa Umma Juu ya Kujiokoa na ...

RAIS MAGUFULI ASIKILIZA KERO ZA WAFANYABIASHARA

Taarifa ya Tafiti mbalimbali zilizofanywa na Wizara ya Habari kuhusu Urithi wa Ukombozi kuwasilishwa kwa mawaziri wa Utamaduni wa nchi za Kusini mwa Afrika Na: Genofeva Matemu - WHUSM Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameahidi kufikisha taarifa ya hatua ambayo Tanzania imefikia katika harakati za kutafiti na kuhifadhi kumbukumbu za ukombozi wa Bara la Afrika kwa mawaziri wa utamaduni wa nchi za kusini mwa Afrika ili nchi hizo wanachama ziweze kuendelea na hatua nyingine ya kuchangia katika ujenzi wa kituo cha kuhifadhi kumbukumbu hizo. Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo Mkoani Mbeya alipofanya ziara kukagua maeneo yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika na kusema kuwa serikali ipo katika mpango ambao maeneo yaliyotumika katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika yatakarabati na kurejesha muonekano wake wa awali ili yasipotezi historia. “Majengo yaliyotumika katika harakati za urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika ni sehemu ya historia na maeneo muhimu sana ambayo yanatakiwa kuboreshwa ili yaweze kuendelea kuwepo katika muonekano ule ule wa awali kwa lengo la kutokupoteza historia yake” amesema Mhe. Mwakyembe Aidha Mhe. Mwakyembe amesema kuwa serikali imechukua wajibu wake wa kubaini maeneo yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika na kuwaomba viongozi wote nchi nzima kuendelea kubaini maeneo na vitu vilivyotumika katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika vilivyopo katika maeneo yao ili wizara iyaendeleze kwa maslahi ya taifa na Afrika kwa ujumla Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Paul Ntinika ameitaka programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kuzingatia na kuchukua taarifa ya vitu mbalimbali kama vile vyakula vilivyotumika, vifaa na nyimbo zilizotumika kuhamasisha ukombozi wa Bara la Afrika ili jamii ya sasa ifahamu kumbukumbu za ukombozi wa Bara la Afrika kwa undani zaidi. Naye Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi. Ingiahedi Mduma amesema kuwa hadi sasa programu inakusanya vitu vyote vilivyotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika ambapo nyimbo 42 zilizokuwa zikihamasisha mambo ya ukombozi zimekusanywa, hotuba 78 zilizotumika wakati wa harakati za ukombozi zimepatikana, maeneo 161 yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi yameainishwa na watu 201 wamehojiwa ambao kwa namna moja ama nyingine wamepitia harakati hizo. Baadhi ya maeneo yaliyobainika Mkoani Mbeya kutumiwa na wanaharakati na wapigania uhuru wa Bara la Afrika ni pamoja na eneo la Game, Nyumba ya Binti Matola, Nyumba ya Juma Mtoto, Uwanja wa Mikutano, Sekondari ya Samora Michel, Nyumba iliyopo Iyela iliyotumiwa na Samora Michel pamoja na Nyumba za kwa Mapunda.

RAIS DKT MAGUFULI AENDESHA MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO 1, t10, t14, Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018 t2: Sehemu ya Viongozi wa serikali na wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018 t6: Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili kuendesha mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018. Kulia kwake ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Joakim Mhagama na kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel t7: Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Dkt. Reginald Mengi alipowasili kuendesha mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018. t8: Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Joakim Mhagama na kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Dkt. Reginald Mengi akijiandaa kufungua mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018. t23, t24 na t25: Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendesha mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018. t28, t29 na t30: Sehemu ya wafanyabiashara wakitoa changamoto zao wakati wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018 Picha na IKULU

Pix 1: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Chief wa kihehe Evaristo Sambiligunga Mwambeta alipokutana na machief wa kihehe kuzungumza nao kuhusu namna ya kuhifadhi historia ya ukomboziwa Bara la Afrika kwa vizazi vijavyo jana Mkoani Iringa Pix 2: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na Machief wa kihehe (hawapo pichani) alipokutana nao kuzungumzia namna ya kuhifadhi historia ya ukombozi wa Bara la Afrika kwa vizazi vijavyo jana Mkoani Iringa Pix 3: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kulia) katika picha ya pamoja na machief wa kihehe baada ya kuzungumza nao kuhusu namna ya kuhifadhi historia ya ukomboziwa Bara la Afrika kwa vizazi vijavyo jana Mkoani Iringa Pix 4: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (watatu kushoto) akiwasili katika makumbusho ya Mtwa Mkwawa yaliyopo Kalenga kwa ajili ya kuona naoma makumbusho hiyo inavyohifadhi na kuendeleza historia ya shujaa Mkwawa aliyepigana vita vya msituni wakati wa harakati za kuwakomboa wahehe kutoka kwa utumwa wa wajerumani jana Mkoani Iringa. Watatu kulia ni Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi. Ingiahedi Mduma Pix 5: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) akiangalia fuvu la Mtwa Mkwawa alipotembelea makumbusho ya Mkwawa yaliyopo Kalenga kwa ajili ya kuona naoma makumbusho hiyo inavyohifadhi na kuendeleza historia ya shujaa Mkwawa aliyepigana vita vya msituni wakati wa harakati za kuwakomboa wahehe kutoka kwa utumwa wa wajerumani jana Mkoani Iringa. Pix 6: Mtaalamu kutoka makumbusho Mkwawa (kulia) akimuonyesha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrion Mwakyembe (wapili kulia) baadhi ya vifaa alivyotumia Mtwa Mkwawa wakati wa harakati za kuwakomboa wahehe kutoka katika utumwa wa wajerumani jana katika makumbusho ya Mkwawa iliyopo katika Halmashauri ya Iringa Mkoa wa Iringa. Pix 7: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa ameshika silaha za jadi alizokuwa anatumia Mtwa Mkwawa wakati wa harakati za kuwakomboa wahehe kutoka katika utumwa wa wajerumani jana katika makumbusho ya Mkwawa iliyopo katika Halmashauri ya Iringa Mkoa wa Iringa. Pix 8: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiangalia kaburi la Mtwa Abdul Adam Sapi Mkwawa alipotembelea makaburi ya machief kutoka ukoo wa Mkwawa jana katika makumbusho ya Mkwawa iliyopo katika Halmashauri ya Iringa Mkoa wa Iringa. Pix 9: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Muungano iliyopo katika mnara wa Frelimo alipotembelea mnara wa Frelimo uliojengea na serikali ya Tanzania mwaka 1977 kwa lengo la kutoa heshima na kumbukumbu kwa aliyekuwa kiongozi wa chama cha ukombozi nchini Mozambiki Bw. Samora Machel. Pix 10: Mwanafunzi kutoka Shule ya Msingi Muungano akijibu swali la kihistoria lililoulizwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa ziara yake katika mnara wa Frelimo ulipo katika shule ya Muungano jana Mkoani Iringa Pix 11: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (watatu kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Halmashauri ya Iringa katika mnara wa Frelimo uliojengea na serikali ya Tanzania mwaka 1977 kwa lengo la kutoa heshima na kumbukumbu kwa aliyekuwa kiongozi wa chama cha ukombozi nchini Mozambiki Bw. Samora Machel. Pix 12: Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Tumaini Dkt. Gibson Sanga (kushoto) akimuonyesha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) baadhi ya vifaa vya kitamaduni vinavyotumiwa na kabila la wahehe alipotembelea makumbusho ya Iringa jana Mkoani Iringa Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM