Posts

Showing posts from June, 2018

MV UMOJA YAZIUNGANISHA TENA UGANDA NA TANZANIA

OPERESHENI NYAKUA NYAKUA

AHADI YA KIVUKO KIPYA YATIMIA MKOANI MWANZA

TUKIO LA WANANDOA WALIOKUTWA WAMEFALIKI SENGEREMA KTK NYUMBA YA WAGENI ...

UPIMAJI SHIRIKISHI WAKOSOLEWA MWANZA

POLISI JIJINI MWANZA WAKAMATA PIKIPIKI 100

TCRA Yasisitiza Matumizi Sahihi ya Mtandao, Kufuata Sheria na Taratibu z...

UBORESHAJI VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI KWIMBA

UJENZI BARABARA YA KISEKE BUSWELU KUANZA RASMI

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA MASHINDANO YA UMISETA TAIFA MWANZA

MACHINGA WALIOVAMIA MAENEO YA MADUKA MWANZA WATAKIWA KUFUATA MAKUBALIANO...

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii katika kutangaza huduma na shughuli mbalimbali za Serikali kwa Maafisa Habari na Maafisa Tehama kutoka Taasisi mbalimbali Serikalini pwakati wa mafunzo maalum yaliyofanyika leo Ijumaa Juni 8, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Mfumo Mpya wa Malipo Mamlaka za Serikali za Mitaa Kuboresha Huduma kwa Wananchi. Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma. Mfumo mpya wa malipo epicor toleo Na. 10.2 unaotarajiwa kuanza kutumika Julai 1 mwaka huu na Mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini umeelezwa kuboresha huduma kwa wananchi kutokana na kuwa wa uwazi na kurahisisha kazi kwa watumiaji wa mfumo huo. Akieleza lengo la uboreshaji wa mfumo huo leo, Jijini Dodoma wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa Manunuzi kutoka Halmashauri za Mikoa ya Kigoma, Shinyanga, Dodoma, Arusha, Manyara na Singida, mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Agustino Manda amesema mfumo huo utapunguza kazi na kuongeza ufanisi wa kazi kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa hapa nchini. “Mfumo huu utaweka mambo wazi, watu watawajibika na mtumiaji wa mwisho ambaye ni mteja atapata huduma nzuri na kuridhika na huduma atakayopewa,” amesema Manda. Ameendelea kusema, lengo la kuboresha mfumo huo ni kutoa huduma nzuri kwa Wananchi, Wananchi kutocheleweshewa huduma, Halmashauri husika kuwa katika nafasi nzuri ya kutoa huduma pamoja na kukusanya mapato vile ilivyotarajiwa. Aidha amewataka Maafisa Manunuzi hao kutoa maelekezo mazuri kwa wateja wao namna mfumo huo unavyofanya kazi ili wateja waweze kuelewa na kuridhika na huduma wanazohitaji. Manda amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kupitia mifumo mbalimbali ya kielektroniki inayoendelewa kuboreshwa hapa nchini wamefanikiwa kupunguza gharama za watumishi kusafiri kwenda Makao Makuu ya Serikali kufuata huduma mbalimbali. Ametolea mfano wa Mfumo wa Kielektroniki wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali za Mitaa (PlanRep) kuwa umewezesha Halmashauri kuandaa bajeti zao wakiwa katika ofisi zao tofauti na awali, ambapo walilazimika kusafiri kwenda Dar es Salaam au Dodoma. Hivyo mradi huo umeipunguzia Serikali gharama za kuwalipa watumishi hao wanapokuwa nje ya vituo vyao vya kazi. Kwa upande wa Meneja Mradi wa PS3 Dodoma, Bw. Gideon Muganda amesema PS3 itaendelea kushirikiana na Serikali kwa ukaribu kuhakikisha mifumo mbalimbali ya sekta za Umma inaboreshwa hapa nchini. Mfumo wa malipo epicor 10.2 utatoa taarifa zote zinazohusiana na fedha katika Halmashauri husika ikiwemo mapato, matumizi pamoja na bajeti ya Halmashauri. Mafunzo ya Mfumo huo yanaendelea kutolewa katika vituo sita ambavyo ni Dodoma, Mwanza, Mtwara, Iringa, Kagera na Mbeya ambapo yamehusisha watumiaji wa mfumo huo ambao ni Waweka Hazina, Wahasibu, Maafisa TEHAMA, Maafisa Manunuzi na Wakaguzi wa Ndani kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo wa namna ya kutumia mfumo huo hasa katika maeneo yaliyoboreshwa. Mafunzo hayo yanafanyika kwa wiki tatu ambapo yameanza Juni 4 na yanatarajiwa kumalizika Juni 21, mwaka huu.

Pix 1:Mtaalamu Mshauri wa masuala ya rasiliamali fedha kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Bi Hellen Nyagwa akifunga Mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) kwa wahasibu,waweka hazina na maafisa usimamizi wa fedha wa mikoa ya Tanga,Iringa na Morogoro yaliyokuwa yakifanyika Mkoani Iringa. Pix 2: Mtaalamu Mshauri wa masuala ya rasiliamali fedha kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Bi Hellen Nyagwa(Aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wahasibu na waweka hazina wa Mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) kutoka Morogoro na Iringa mara baada ya kufunga mafunzo hayo. Pix 3: Mtaalamu Mshauri wa masuala ya rasiliamali fedha kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Bi Hellen Nyagwa(Aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wahasibu na waweka hazina wa Mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) kutoka Tanga mara baada ya kufunga mafunzo hayo. Pix 4:Afisa TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw.James Mtatifikolo akitoa mada jinsi ya kutumia dawati la Msaada kwa watumiaji wa mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la Epicor 10.2 kwa wahasibu,waweka hazina na maafisa usimamizi wa fedha wa mikoa ya Tanga,Iringa na Morogoro. Picha na Daudi Manongi,MAELEZO,IRINGA

WISN na POA Kuimarisha Huduma za Afya Katavi Na: Frank Mvungi - MAELEZO, Mbeya Mkoa wa Katavi umetajwa kunufaika na mfumo wa kubaini taarifa za mahitaji ya watumishi kwa kuzingatia uzito wa kazi, ambapo Halmashauri zote 185 na Mikoa yote Tanzania bara inanufaika na mifumo hiyo inayolenga kuimarisha huduma za afya. Akizungumza leo Jijini Mbeya wakati akifungua mafunzo kwa makatibu wa afya, maafisa utumishi, wataalamu wa takwimu za afya, na waganga wakuu wa Wilaya wa mkoa wa Katavi, Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Utawala na Rasilimali Watu wa mkoa huo, Bi. Crescencia Joseph, amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuzijengea uwezo Halmashauri na Mikoa ili ziweze kutumia mifumo ya WISN na POA iliyorahisishwa kuwapangia vituo vya kazi, na katika kuomba watumishi wapya kulingana na mahitaji. WISN ni mfumo unaotumika kubaini mahitaji ya watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya na vipaumbele katika maeneo husika, Wakati POA hutumika kupanga mgawanyo wa watumishi hao kulingana na uhitaji wa kila kituo, Mifumo hii miwili iko chini ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), pamoja na Ofisi ya Rais – Utumishi, kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID). Mradi huu wa miaka mitano unatekelezwa katika mikoa 13 ya Tanzania bara. “Serikali kupitia OR-TAMISEMI inatarajia kuajiri watumishi wapya 6180 wa sekta ya Afya na 1500 kutoka Wizara ya Afya, hivyo ni matarajio yangu kuwa halmashauri zitatumia ripoti za mfumo wa WISN na POA iliyorahisihwa katika kugawanya watumishi wapya kwa kuzingatia taarifa za mifumo hiyo,” alisisitiza Bi. Crescencia. Akifafanua, amesema kuwa mifumo hiyo ni ukombozi mkubwa katika kutoa huduma za afya katika maeneo yote hasa yale yaliyo pembezoni, kwakuwa itasaidia kuimarisha huduma zinazotolewa kwa wananchi. Aidha, Bi. Crescencia aliwaasa washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia yale watakayojifunza ili waweze kwenda kuwatumikia wananchi katika kutoa huduma bora na zenye tija kama ilivyo dhamira ya Serikali. Pia aliipongeza OR-TAMISEMI Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mradi wa PS3 kwa kutoa mafunzo ya mfumo wa WISN na POA kwa mikoa ya Mwanza, Mara, Iringa, Tanga, Mbeya, Kigoma, Morogoro, Pwani na Mtwara. Mifumo ya WISN na POA iko chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Ofisi ya Rais Utumishi, ikiwa ni moja ya hatua zinazochukuliwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kuboresha huduma za afya hapa nchini.

Wahasibu wa Halmashauri za Mikoa ya Dodoma na Singida Waendelea Kunolewa Namna ya Kutumia Mfumo Mpya wa Malipo Epicor 10.2.

Baada ya Msiba wa Mapacha Walioungana Maria na Consorata, Mapacha Wengin...

WANAMWANZA WAASWA KUDUMISHA UMOJA NA UDUGU ULIOPO ILI KUENZI MISINGI YA...

MACHINGA MWANZA WAVAMIA VIBARAZA VYA MADUKA KUPANGA BIASHARA