Posts

Showing posts from April, 2018

Waliosema Mwenge Uwekwe Makumbusho Hawajui Shughuli za Mwenge

Vitabu laki 5 vya Kufundishia Kugawiwa Shule za Msingi,

Chanjo ya Saratani ya Shingo ya Kizazi Yaendelea Kutolewa

RAIS JOHN POMBE MAGUFULI WALIOKULA PESA ZA MRADI WA MAJI KONDOA KUSAKWA

Taarifa ya Utekelezaji Miradi Halmashauri ya Jiji la Mwanza

Balaza la Madiwani Kikao cha Tatu MWANZA

RPC MWANZA AWAONYA WATAKAO JARIBU KUANDAMANA

NGOMA YA KUCHEZA NA NYOKA

RAIS MAGUFULI AKERWA NA UPOTOSHAJI JUU YA UPOTEVU WA TRILIONI 1 5

TAKUKURU , MBUNGE MSTAAFU ATIWA MBARONI NA TAKUKURU

Bank ABC Yaahidi Mapinduzi ya Kibiashara

ZIMAMOTO YANUSURU MAISHA YA MTU MMOJA ALIYE UNGULIWA NA NYUMBA

Rais Magufuli awatembelea wagonjwa wa moyo

Siku ya watoto wanaoshi mtaani na kufanya kazi mtaani

MABINTI MIAKA 9 HADI 14 KUPATIWA CHANJO YA SARATANI MLANGO WA KIZAZI

MADIWANI ILEMELA NA NYAMAGANA WAPIGWA MSASA KATIKA UTENDAJI

SILAHA, WAHALIFU WAKAMATWA OPERESHENI YA POLISI

SILAHA, WAHALIFU WAKAMATWA OPERESHENI YA POLISI. Na. Jeshi la Polisi. Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kukamata Silaha mbalimbali na watuhumiwa 368 katika Oparesheni Maalum inayoendelea katika Ukanda wa Kusini unaojumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma. Akizungumza mkoani Mtwara, Mkuu wa Operesheni Maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema kati ya watuhumiwa 368, 13 tayari wamefikishwa Mahakamani, 152 wamekabidhiwa Idara ya Uhamiaji kwa hatua zaidi, tisa wapo chini ya Upelelezi na 194 wapo chini ya uangalizi wa Polisi (Police Supervisee). Sabas amezitaja Silaha zilizokamatwa kuwa ni pamoja na SMG mbili, Pistol tano, Shotgun moja na risasi 145, Visu 96, Makoti ya Sare za Jeshi la Msumbiji mawili, Raba za Jeshi la Msumbiji jozi mbili pamoja na vifaa vya kutengenezea milipuko. “Baadhi ya watuhumiwa ni wale waliokimbia katika Operesheni yetu ya Mkoa wa Kipolisi Rufiji baada ya kuwazidi nguvu na sasa nawaambia tu wajisalimishe kwani hatuna mchezo hata wakimbilie wapi mana tumepata taarifa kuwa wamejificha nchini Msumbiji lakini kule napo wameanzisha operesheni kama hii“. Alisema Sabas. Aidha Kamanda Sabas amesema Operesheni hiyo ni endelevu na inashirikisha vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama hivyo ametoa wito kwa raia wema kuendelea kutoa taarifa za siri ili kuendeleza amani na usalama hapa nchini. Hivi karibuni Mkuu wa Jeshi la Polisi la nchini Msumbiji alikutana na IGP Simon Sirro jijini Dar es Salaam kwa lengo kuboresha ushirikiano katika mapambano ya uhalifu unaovuka mipaka ambayo ndio imekuwa changamoto katika nchi mbalimbali.

MAMIA WAOMBOLEZA MSIBA WA BABA WA MBUNGE WA ILEMELA MWANZA

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA WAOMBOLEZA KUAGA MWILI WA MZEE SYLVESTER LUBALA SHIMBA, BABA MZAZI WA NAIBU WAZIRI ANGELINA MABULA

Rais Dkt. Magufuli azindua rasmi taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF)

MKUTANO MKUU WA JIMBO LA ILEMELA TAARIFA YA UTEKELEZAJI ILANI YA UCHAGU...

MBUNGE WA ILEMELA AZINDUA UJENZI KIWANGO CHA LAMI BARABARA KM 3 IBANDA

MKUU WA MKOA MWANZA AVUNJA MKATABA WA UKARABATI VITUO VYA AFYA BUCHOSA

Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kushirikishwa katika Tuzo za The African Prestigious Awards Na Anitha Jonas – WHUSM 09/04/2018 Dar es Salaam. Utendaji uliyotukuka wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na ukuwaji wa sekta ya filamu nchini ndiyo vinavochangia kuitangaza nchi yetu katika tuzo za The African Prestious Awards. Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akimkabidhi bendera msanii wa filamu nchini Yvonne Cherrie Maarufu kama Monalisa anayetarajia kwenda nchini Ghana katika tuzo hizo. “Tanzania imepata heshima kubwa katika tuzo hizi zenye heshima kubwa katika bara la Afrika ambapo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ameteuliwa kuwania Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika, napia tuna wasanii watatu ndani ya tansia ya filamu ambao ni King Majuto anayewania Tuzo ya Mchekeshaji Bora Afrika,Raymond Kigosi anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika na Monalisa mwenyewe anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika pamoja na Mpiga picha Mahiri Moiz Hussein anayewania Tuzo ya Mpiga Picha Bora Afrika,”alisema Dkt.Mwakyembe. Akiendelea kuzungumza katika sherehe hiyo ya kukabidhi bendera Mheshimiwa Mwakyembe aliwasisitiza wasanii wanchini kuendelea kuandaa kazi zinazoonyesha ubunifu wao kwani ukuaji wa tansia ya filamu Tanzania uko mikononi mwao na si vinginevyo. Pamoja na hayo nae Msanii wa Filamu nchini Yvonne Cherrie Maarufu kama Monalisa anayetarajia kuondoka nchini mapema wiki hii kwenda nchini Ghana kwa ajili ya Tuzo hizo aliwaahidi watanzania kuwa lazima atarudi na tuzo kwani anawawakilisha wasanii wenzake hao wawili pamoja na mpiga picha huyo aliyetajwa na pia aliishukuru serikali kwa kumpatia tiketi kwa ajili ya kufanikisha safari hiyo. “Tuzo hizi nazichukulia kama ni heshima kubwa sana kwangu kwani kipengele ninachowania kinahusisha wasanii wakubwa katika bara la afrika kwani niko pamoja na Lupita Nyongo ambaye ni mwigizaji wa Hollywood pamoja na Jackie Apia ambaye nae anafanya vizuri hivyo hata nisipopata tuzo hii kwangu kuchaguliwa kwanza katika kipengele hicho tayari ni ushindi kulinga na uwezo wasanii wenzangu tuona shindana,”alisema Monalisa. Kwa upande wa Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini Bibi.Joyce Fissoo alisema anafurahishwa kuona sekta ya filamu ya nchini ikikua na kuleta taswira mpya katika bara la afrika ambapo wasanii watanzania nao kazi zao zinavuka mipaka na kuleta changamoto katika ushindani katika tasnia filamu Afrika. Hata hivyo nae mama mzazi wa Monalisa Bibi.Suzan Lewis maarufu kama Natasha alieleza kufurahishwa na kazi ya filamu anayoifanya mwanaye na pia alieleza kuwa anamtakia mafanikio makubwa pamoja na kushinda tuzo hiyo. ***********Mwisho************

T P A KUAZIMISHA MIAKA 13 JIJINI MWANZA

WAZIRI MWAKYEMBE AWAASA WATANZANIA KUPAMBANA NA VIASHIRIA VINAVYO SABABISHA MAUAJI YA KIMBARI Na: Mwandishi wetu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, amewaasa Watanzania kuhakikisha wanapambana na viashiria vyote vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani na mauaji ya kimbari. Kauli hiyo Dkt. Mwakyembe ameitoa wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu za mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda miaka 24 iliyopita. Kwenye hotuba yake Dkt. Mwakyembe amesema mauaji ya kimbari hayatokei ghafla bali huanza kwa chokochoko na kauli za kichochezi ambazo zina lengo la kuigawa jamii vipande vipande. “Kilichotokea Rwanda ni fundisho kwetu, mauaji ya kimbari hayatakiwi kutokea tena. Kuhakikisha hayatokei lazima tuyadhibiti mambo yote yanayoweza kuligawa taifa kwa faida ya kizazi cha leo, kesho na keshokutwa” Dkt. Mwakyembe alisisitiza. Kuendelea kutia mkazo wa ujumbe wake Dkt. Mwakyembe aliinukuu kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, aliyoitoa wakati wa ziara yake ya kikazi nchini Rwanda ambapo alisema “haya hayatatokea tena, hatuwezi kubadili kilichotokea awali, lakini tunaweza kubadilisha hali ya leo na hata ya baadae”. Balozi wa Rwanda nchini mheshimiwa Eugine Kayihura ameishukuru Serikali na wananchi wa Tanzania kwa kuendelea kuwa pamoja na Wanyarwanda. Pia ameahidi kuendeleza ushirikiano wa kindugu kati ya Tanzania na Rwanda kwa maendeleo ya watu wake. Kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez amesema nchi zote zina wajibu wa kuwalinda wananchi wake dhidi ya mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. Pia zinatakiwa kuhakikisha zinaungana kupambana na mtu au kikundi chochote chenye nia ya kutekeleza uhalifu kama huo. Kumbukumbu za mauaji ya kimbari ya Rwanda huadhimishwa kila mwaka na mwaka huu maadhimisho hayo kwa Tanzania yamefanyika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City ambapo Dkt. Mwakyembe alikuwa mgeni rasmi. Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, watu mashuhuri, viongozi wa serikali na mashirika ya kimataifa na wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Dar-es-salaam.

RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA KUMSIMIKA MHASHAMU ISAACK AMANI KUWA ASKOFU MKUU JIMBO LA KATOLIKI ARUSHA LEO

RAIS MAGUFULI AAGIZA POLISI KUTOKATA BANGI BADALA YAKE WALIOLIMA NDIO WA...

RAIS DKT MAGUFULI ASHUHUDIA ASKARI POLISI KATIKA MAZOEZI YA KUPAMBANA NA WAANDAMANAJI NA MAGAIDI KATIKA SIKU YA KARUME JIJINI ARUSHA

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA KITUO CHA POLISI CHA DIPLOMASIA NA UTALII NA MAKAZI YA POLISI JIJINI ARUSHA LEO

Serikari Yatoa Mil 100 kwa Mvumbuzi wa TANZANITE Mzee Jumanne Ngoma

Mawe ya Mwanza Yawashangaza Wanafunzi wa Skuli ya Kangani Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mzee Jumanne Ngoma, mvumbuzi wa madini ya Tanzanite, wakati wa uzinduzi rasmi wa ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la mgodi wa madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA UKUTA ENEO LA MGODI WA TANZANITE MIRERANI MKOANI MANYARA LEO m19:" Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya shukrani Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo baada ya jeshi hilo kukamilishi mbele ya wakati ujenzi wa ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la mgodi wa madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018 m20: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi kitambulisho cha Taifa mmoja wa wamiliki wa migodi ya Tanzanitehati ya shukrani Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Jenerali Venance Mabe ili kuwawezesha kupata ruksa ya kuingia na kufanya kazi ndani ya eneo lililozungukwa na ukuta eneo la mgodi wa madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018 m21: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifunua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la mgodi wa madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018 m29: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli na viongozi wengine wakipata maelezo ya madini ya Tanzanite yanavyochajkatwa wakati wa uzinduzi rasmi wa ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la mgodi wa madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018 m31: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli na viongozi wengine katika picha ya pamoja na watendaji wa JWTZ na JKT waliosimamia kazi za ujenzi wa ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la mgodi wa madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018 m39: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli katika picha na mvumbuzi wa madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Ngoma wakati wa uzinduzi rasmi wa ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la mgodi wa madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018 Picha na IKULU

Kamati ya Bunge Yasikitishwa na Vyoo vya Sekondari ya Bwiru Girls

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO. Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kufanya utafiti wa taarifa wanazozitengeneza kabla hawajazitoa kwa jamii kupitia vyombo vya habari. Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi ametoa rai hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga mafunzo ya Waandishi wa Habari za maendeleo yaliyotolewa na Wakfu wa Tasnia ya Habari Tanzania (TMF) juu ya usalama barabarani pamoja na masuala ya maendeleo. Dkt. Abbasi amesema kuwa Waandishi wa Habari wanatakiwa kufahamu haki na wajibu wa taaluma hiyo ambapo moja wapo ya wajibu wa mwanahabari ni kufanya utafiti wa chanzo na habari husika kabla ya kuifikisha kwa jamii ikiwa ni njia itakayosaidia kuzuia utoaji wa habari zisizo na uhakika kwa jamii. "Kutoa taarifa za uhakika kwa jamii kunahitaji taaluma na weledi wa hali ya juu, hivyo Wanahabari wanatakiwa wajikite zaidi katika kutafuta taarifa sahihi na kusisambaza kwa wananchi. Nawapongeza sana TMF pamoja na wadau wote walioshiriki katika uandaaji wa mafunzo haya." amesema Dkt. Abbasi. Dkt. Abbasi amefafanua kuwa Waandishi wa Habari wana haki ya kuikosoa Serikali ambapo Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 katika kifungu cha 52 (2) imebainisha suaka hilo lakini taaluma, weledi haki na wajibu katika uandishi wa habari lazima vifuatwe. Amewaomba wafadhili wa mafunzo hayo pamoja na wadau wengine kutochoka kuwasaidia wanahabari ili waweze kutimiza majukumu yao ya kutoa taarifa kikamilifu na kuendelea kuwa washirika wa maendeleo nchini. Kwa upande wake Mkurugenzi wa TMF, Fausta Msokwa amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari kuwa wabobezi katika kutoa taarifa za uhakika za masuala mbalimbali ya maendeleo. "Mafunzo hayo yameleta uhai endelevu katika tasnia ya habari na kuwafanya Waandishi wa Habari kutoa habari zenye tija hasa katika kuelezea changamoto zilizopo maeneo ya vijijini," amesema Mkurugenzi Fausta. Mafunzo hayo yaliyoanza mwezi Mei mwaka jana na kuhusisha waandishi wa habari 15, yamefanyika kwa ushirikiano wa Wakfu wa Tasnia ya Habari Tanzania, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na baraza la usalama barabarani na kufadhiliwa na Shirika la Afya Duniani pamoja na Taasisi ya Bloomberg. CAPTIONS 1. Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa Waandishi wa Habari aliyefanya vizuri katika mafunzo hayo, Adelina Bosco wakati wa kufunga mafunzo ya Waandishi wa Habari yaliyotolewa na Wakfu wa Tasnia ya Habari Tanzania (TMF) juu ya usalama barabarani pamoja na masuala ya maendeleo.Ufungaji huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam. 2. Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa Waandishi wa Habari aliyepata tuzo zijulikanazo kama 'simema zetu' kwa kuandaa makala bora za Televisheni,Anwaly Msechu wakati wa kufunga mafunzo ya Waandishi wa Habari yaliyotolewa na Wakfu wa Tasnia ya Habari Tanzania (TMF) juu ya usalama barabarani pamoja na masuala ya maendeleo.Ufungaji huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam. 3. Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wadau, washiriki na wakufunzi baada ya kufunga mafunzo ya Waandishi wa Habari yaliyotolewa na Wakfu wa Tasnia ya Habari Tanzania (TMF) juu ya usalama barabarani pamoja na masuala ya maendeleo.Ufungaji huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.