Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kushirikishwa katika Tuzo za The African Prestigious Awards Na Anitha Jonas – WHUSM 09/04/2018 Dar es Salaam. Utendaji uliyotukuka wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na ukuwaji wa sekta ya filamu nchini ndiyo vinavochangia kuitangaza nchi yetu katika tuzo za The African Prestious Awards. Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akimkabidhi bendera msanii wa filamu nchini Yvonne Cherrie Maarufu kama Monalisa anayetarajia kwenda nchini Ghana katika tuzo hizo. “Tanzania imepata heshima kubwa katika tuzo hizi zenye heshima kubwa katika bara la Afrika ambapo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ameteuliwa kuwania Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika, napia tuna wasanii watatu ndani ya tansia ya filamu ambao ni King Majuto anayewania Tuzo ya Mchekeshaji Bora Afrika,Raymond Kigosi anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika na Monalisa mwenyewe anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika pamoja na Mpiga picha Mahiri Moiz Hussein anayewania Tuzo ya Mpiga Picha Bora Afrika,”alisema Dkt.Mwakyembe. Akiendelea kuzungumza katika sherehe hiyo ya kukabidhi bendera Mheshimiwa Mwakyembe aliwasisitiza wasanii wanchini kuendelea kuandaa kazi zinazoonyesha ubunifu wao kwani ukuaji wa tansia ya filamu Tanzania uko mikononi mwao na si vinginevyo. Pamoja na hayo nae Msanii wa Filamu nchini Yvonne Cherrie Maarufu kama Monalisa anayetarajia kuondoka nchini mapema wiki hii kwenda nchini Ghana kwa ajili ya Tuzo hizo aliwaahidi watanzania kuwa lazima atarudi na tuzo kwani anawawakilisha wasanii wenzake hao wawili pamoja na mpiga picha huyo aliyetajwa na pia aliishukuru serikali kwa kumpatia tiketi kwa ajili ya kufanikisha safari hiyo. “Tuzo hizi nazichukulia kama ni heshima kubwa sana kwangu kwani kipengele ninachowania kinahusisha wasanii wakubwa katika bara la afrika kwani niko pamoja na Lupita Nyongo ambaye ni mwigizaji wa Hollywood pamoja na Jackie Apia ambaye nae anafanya vizuri hivyo hata nisipopata tuzo hii kwangu kuchaguliwa kwanza katika kipengele hicho tayari ni ushindi kulinga na uwezo wasanii wenzangu tuona shindana,”alisema Monalisa. Kwa upande wa Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini Bibi.Joyce Fissoo alisema anafurahishwa kuona sekta ya filamu ya nchini ikikua na kuleta taswira mpya katika bara la afrika ambapo wasanii watanzania nao kazi zao zinavuka mipaka na kuleta changamoto katika ushindani katika tasnia filamu Afrika. Hata hivyo nae mama mzazi wa Monalisa Bibi.Suzan Lewis maarufu kama Natasha alieleza kufurahishwa na kazi ya filamu anayoifanya mwanaye na pia alieleza kuwa anamtakia mafanikio makubwa pamoja na kushinda tuzo hiyo. ***********Mwisho************





Comments