HASHIKOME CHANNEL MPYA.
barmedas.tv kwa kutambua  Tanzania inauenzi utamaduni na mila za muafrika, barmedas.tv imechukua hatua ya kuanzisha channel itakayohusika na utamaduni husisani wa Makabila yaliyoko Kanda ya Ziwa Victoria.
barmedas.tv inaheshimu watazamaji wake ni watu wanapenda vipindi mbali mbali na ndio maana ikatenga channel mbali mbali oli kukidhi haja za watazamaji wake mfano inekuwa na channel zofuatazo:
1. barmedas - channel inayojihusisha na vipindi vya kijamii.
2.HeaveN - mambo ya dini
3.24/7 Sports -Michezo
4.Africana- Move zilizotafasiriwa za kihindi na Kinaigeria.
5.Muzika - channel inayokuruhusu kuchagua wewe mwenyewe wimbo uupendao na kuiagiza ikupigie wimbo huo na hii channel inafanya.
6.MTG- channel inayotangaza biashara na taarifa zote katika Jiji la Mwanza
7.Latest Movie- Channel inayokupa Film zilizobuma na kupendwa enzi zile
8.Hatimae Hashikome- channel inayohusika na masuala ya mila utamaduni na desturi.
Akiongea Maneja wa Vipindi (Programe Manager)  alipoulizwa madhumuni ya kuanzisha channel hii Ndg Sokoro alisema, lengo la barmedas tangu awali nikukidhi haja ya msikilizaji na ndicho wamekifanya tangia awali na ndio wana kauli mbiu yao (Slogan)  "Sisi tunatangulia na wengine wanafuata" tukiwa na maana kuwa kila tunachokuwa tunakifanyia kazi pasipokuchelewa na ndipo utakuta wengine mpaka wakatupate malengo yetu sisi tuko mbali.
Tumekuwa na kipindi kinaitwa hashikome huendeshwa na barmedas kila siku ya Alhamis kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 2:00 usiku nikipindi cha saa 2 lkn kimekuwa kipindi kama kifupi jinsi gani mambo mazuri hufanyika humo nakupelekea kila mara wageni na watazamaji kwa ujumla hupenda mda uongezwe basi Wakurugenzi qa barmedas waliliona hilo na wakaridhia sasa tuanzishe Channel ili ifanye mengi katika channel hii na watu watakumbuka kwa maana sasa ukiangalia mila na desturi za.Mtanzania zinaenda zinapungua hadhi yake hivyo basi,  chombo hicho kitajaribu kuhamasisha na kuwatumia wadau watakao weza kuweka nguvu zaidi katika Channel hii.
Mategemeo ya Channel hii itazinduliwa mapema siku ya Jumanne na kiongozi bado tunawasiliana nae Kwani shughuli hii yote tuko sambamba na kituo cha Makumbusho Bujora,  ambapo tumeamua kufanya kazi kwa pamoja na ndio maana , hata sherehe hizi za bolabo, barmedas.tv wameratibu matukio yote tangu siku ya 1 hadi siku ya mwisho.
Akijibu swali la kuwa hivyo baada ya uzinduzi channel itaanza lini Sokoro alisema kila kitu kiko tayari wakati wowote itaanza kurusha vipindi vyake vya utamaduni " hivi sasa navyozunguma nanyi tayari vifaa vya channel hii vimesha fika baada ya Mkurugenzi alikuwa kavifuata  nje ya nchi.
Aliwataka watazamaji sasa na wapenzi wa nyimbo za asili ni wakati wao sasa kuleta nyimbo zao lakini hata matangazo yao ili biashara zao ziuzike kupitia pia channel hii " si munajua  tena , biashara ni matangazo?" alimaliza kusema Manager huyo.

Channel hiyo ya Hashikone itazinduliwa huko Bujora na kushuhudiwa na wazee wa mila na desturi za Kisukuma ina maana, watakuwepo Watemi, viongozi wa Chama na Serikali , Wadau mbali mbali, viongozi kutoka barmedas, Waandishi wa habari na wageni waalikwa vile vile na mgeni rasimi atakae izindua Channel hii.

Comments