KANDA YA ZIWA-barmedas.tv


KANDA YA ZIWA  YAMALIZA NAFASI YA SABA UMISETA.

Kikosi cha Kanda ya ziwa kimemaliza nafasi ya saba Kitaifa katika mashindano ya umoja wa Michezo kwa shule za Sekondari Tanzania  ( UMISETRA). yaliyomalizika huko Kibaha - Pwani.

Kanda ya ziwa ilicheza Mechi asaba ikashinda michezo  mitano ikafungwa miwili , huku  timu ya soka ya Wanaume ilitinga  hatua ya nusu fainali dhidi ya Kanda ya Mashariki na kufungwa  2-1 , ikacheza na Kanda ya kati kutafuta mshiindi wa tatu, ikaashinda 4-1.

Kanda ya ziwa imetwaa vikombe viwili vya soka Wanaume mshindi wa tatu,  riadha Wanawake , mshindi wa pili, hivyo kushika nafasi ya saba kitaifa kati  ya 12,  huku Kanda ya mashariki ikiibuka kinara.

Comments