MCHOPA CUP- barmedas.tv


MCHOPA  CUP 2014.

Kombe la Kumbu kumbu ya marehemu Osward Mchopa Simon Mchopa "Mchopa Cup"
limeanza kutimua vumbi katika uwanja wa Nyamanoro, kwa kuzishirikisha timu  sita toka Wilaya ya Nyamagana  Mkoani-  Mwanza.

Kombe hilo ambalo ni mara ya kwanza , linazishirikisha timu za Marsh Athletics,River Side,Barcelona,Liberty shooting, FFU Police,Black Star aliyeiacha marehemu  Mchopa, enzi za uhai wake alikuwa akiinoa pia timu hii.

Zawadi zitakazo tolewa ni pamoja na ng'ombe mwenye thamani ya Shilingi laki nne na nusu, kwa atakae kuwa mshindi wa Kwanza, na mshindi wa pili atapata vifaa vya michezo.

Marehemu Osward  Mchopa ambae pia alikuwa Katibu msaidizi wa Chama cha Mpira, kocha msaidizi wa soka la Vijana Mkoani hapa na Kocha Mkuu u-zo ya Toto,alifariki  Juni  9 ,2012 na kuacha mjane na watoto 3. "Bwana alitoa na Bwana alitwaa Jina lake litukuzwe" -AMEN

Comments