SHEREHE ZA BULABO-barmedas.tv

Sherehe hizi za ngoma ya Kisukuma ambazo kila Mwaka hufanyika mara moja na kipindi hicho huwa cha Mavuno, watu wanakuwa wanavuna /wamevuna mazao yao.
Wasukuma wanaamini sherehe hizi hujumuisha
nakuwakutanisha ndg marafiki na mahasimu ambao hutambiana kuhusiana na mapato ya Mwaka huo, pia ni fursa nzuri kutambuana na hata ndoa katika kipindi hiki hufanyika kwani Mahari hupatikana kutokana na mavuno yanayotokana na kilimo ama biashara.

Kipindi hiki ngoma hutawala kila pahali pia zikiambatana na nyimbo za majigambo na wakati mwingine mzee kwenye kijiji anaweza kutukana ama kusema maneno yanauokiudhi kikundi na yy hupewa faini ( Ihyu) na yeye hulipa papo hapo , ngoma huvutia wakati zikipigwa na wahusika huonyedha umahiri mkubwa sana.

Mwaka huu umekuwa wa aina yake kwa kupata sapoti kutoka kwenye Makampuni makubwa likiwemo kituo cha utangazaji, barmedas.tv  Makampuni ya Bia nakadhalika , pia kuonyesha kombe la dunia Live,  watu walifurahia sana kitu hicho.

Mwaka huu tunashuhudia kwa macho muiyikio wa watu tofauti na Miaka iliyopita maana kulionyesha sherehe hizo zilikuwa zikisua sua na kudorora  kabisa. Watu wameonyesha vipaji vya hali ya juu kushiriki katika mashindano ambayo yalikuwa yakiwavuta wstazamaji waliofika kwenye Tamasha hilo.

Comments