VILLA PARK RESOLT-barmedas.tv

SUPER KAMANYOLLA BAND

Band yenye masikani yake hapa Mwanza na shughuli zake huzifanya katika Ukumbi wa Villa Park ulioko kando kidogo Mjini kati, Ukumbi huu uko katika kitongoji maarufu kinaitwa Kirumba.

Band hii ilihamishia makazi yake Mwanza kwa Wapigaji wake waliokuwa wakipiga katika Band mbali mbali zilizoko hapa Nchini na nje ya Nchi.

Band hii hupiga katika ukumbi huu maarufu wenye chakula safi zao la ziwa Victoria na pia Muziki safi wa aina zote utaupata kupitia Band hii ya Super Kamanyolla iliyosheheni wanamziki walio naweredi mkubwa katika Tasinia hii ya Muziki. lakini huwezu kuwakosa kituo cha barmedas.tv wapigapo wana Kamanyoll kwani barmedas.tv ndio huratibu maonyesho yao aidha kwa kurusha Live shoo yao ama kwa kurekodi na baadae kuzirusha katika Channel zao.

Picha chini zinaonyesha jana walikuwa wakipiga show ya mwisho kabla ya kuanza mfungo wa Ramadhani ambapo mwezi unategemewa kuandama leo, na hivyo kupelekea shughuli za Muziki zitasimama hadi pale Waislamu watakapofungua ndi[pi shughuli tena zitaendelea, kwa maana nyingi shughuli za Super Kamanyolla zitasimama hadi Mwezi mzima. barmedas.tv inawatakia Waislamu kote Duniani mfungo wenye Amani na furaha tele katika kutimiza nguzo moja wapo za Kiislamu ambazo huwa nguzo 5.


Comments