MV JUBLEE HOPE- barmedas.tv

Mwl Sokoro akiwa ndani ya  Mv  Jublee Hope baada ya kufika katika  Bandari ya Mwanza  ( Mwanza North Port) Kanisa la AICT Geita limeweza kuleta Meli hiyo itakayofanya kazi ya utibabu katika maeneo ya visiwa ili kupunguza adha ya matibabu kuwa mbali ama visiwa vingine hutewgemea matibabu kutoka kwa Watu walioweza kufungua Zahanati zao binafsi.

Ujio wa Meli hiyo utaleta unafuu mkubwa kwa ajili ya wakazi walioko visiwani kupata matibabu ya haraka na nafuu kwani matibabu yatatolewa bure kwa mjibu wa Ask Mussa Magwesela wa Dioces ya Mwanza na ambaye mradi huu utakuwa kwake aliwaeleza wahudhuliaji waliofika kushuhudia Khafla hiyo fupi.



Comments