ASK JOHN BUNANGO-barmedas.tv

KUTOKA UALIMU HADI UASKOFU:
Nisiku chache zimepita tumeshuhudia Mwalimu aliyekuwa akifundisha chuo cha Biblia Katungulu chuo kilchoko Wilaya ya Sengere,ma Mkoa wa Mwanza Mungu kumujalia hadi kushika nafasi ya juu kabisa katika Kanisa la AICT Maskongoro akiwa Ask wa Dioces nafasi kwa mjibu wa katiba ya Kanisa hilo, haipigiwi kura nikiwa ni na maana anaishika ama afariki dunia ama apatwe na kitu cha kumfanya nafasi yake ibatilishwe.
Kama aliyemtangulia Ask Daniel Nungwana nae alikuwa Mwalimu wa Chuo cha Biblia Cha Nassa, nae kwa mwendo kama huo huo alibahatika Mungu kumchagua kuwa Askofu wa Dioces ya Mwanza na baadae aliweza kuwa Askofu Mkuu wa AICT kwa miaka 8 nafasi aliyoikabidhi kwa Askofu aliyepo sasa Askofu Silas Kezakubi.
Ask John Bunango Nditti, ni majuzi tu alikabidhiwa kijiti cha kuiongoza Dioces ya Mwanza hadi hapo Mungu atakapokuwa amua labda ashike tena mwingine kama Katiba itakavyokuwa ikisomeka sasa ibadirike na kuwa anapigiwa kuraq baada ya mda fulani ukifika kama nafasi ya Ask Mkuu ilivyo sasa.
Askofu John Bunango kwa Historia yake ilivyosomwa Dioces ya Mwanza itakuwa pia imepata Jembe jingine kama Wakrito wa Kanisa hilo na Dioces kwa ujumla walivyoanza kuntaja sasa.
Dioces ina rasilimali nyingi ikiwa pamoja na Kwaya maarufu kama AICT Makongoro Kwaya , Mwanza Town Kwaya na zingine nyingi ambazo zinafanya vizuri sana katika Tanisia hiyo ya Muziki wa Injili.
Nachotaka kusema hivi Ask John Bunango anza Kazi kwa kuangalia mapungufu yaliyokuwa nisugu ili upambane nayo kwani Wakristo wa Kanisa la Makongoro ni watu waliokomaa Kiimani lakini pia wanavipaji vikubwa na ukarimu kwa Viongozi wao.




Comments