KARIBU MWANZA-barmedas.tv

Mwl Sokoro akipiga picha na Mgeni wake Ask Charles Sekelwa alipokitembwlea KITUO cha barmedas katika ofisi zilizoko Mtaa wa Bantu.

Akiongea na Mwenyeji wake, Ask Charles Sekelwa aliwashukuru Wakurugenzi, wafanyakazi wrote pia hakusita kukisifia KITUO cha barmedas Kwa kushiriki moja Kwa moja katika kutoa huduma na TAARIFA za Makanisa lakini pia Kwa kushiriki katika matukip mbali mbali  ya raha na shida.

Pia alikiomba KITUO hiki kipindi hiki cha Christimas KITUO kiwe chachu Kwa kutangaza na kupeleka injili Kwa Watazamaji hasa kipindi cha Christmas.

Mwl Sokoro Kwa niaba ya uongozi wa barmedas alisema  kweli  tayari kila Mwaka hushiriki kikamilifu Kwa ajili ya kurusha Ibada na Watu huweza kuangalia program za majira haya ya Christmas barmedas.tv imekwisha jipanga  kushiriki kikamilifu katika sikukuu ijayo ya Christmas na Mwaka Mpya 2015.

Comments