TANATAZAMA barmedas.tv MTG .

MTG KATIKA KUPASUA MAWIMBI.
 Tulifanya ziara uwanja wa ndege wa Mwanza kuweza kuona huduma zetu katika Uwanja huo wa Ndege wa  Mwanza, kweli ilikuwa kama saa 3:00 tuliondoka Mimi Sokoro, Ashraf na Juma Khamis hadi uwanjani.

Jambo la kufurahisha hali ilikuwa shwari sana na wasafiri walikuwa wakisubiri mda wao ufike waweze kuruka na kuelekea kule  waliko kusudia, kitu cha kufurahisha ni kuwa, Wahudumu wa eneo hilo wote ni wakarimu na walikuwa wakionyesha sura ya furaha wakati wote,  tuliwasalimia na kuwauliza mfanyakazimwenzetu  anae hudumia hapo kuangalia Screen 1. Kama zinafanya kazi bara bara pasipo kuzimika zimika
2. Kama Screen zote ni safi hazina mavumbi wala tando za Bui bui.
3.Kama zinaonekana vizuri pasipo Mchele mchele wala chenga chenga.
hakika mwenyeji wetu tulimpata na akaweza kutuzungusha kwa kuwa alikuwa amewajulisha wafanya kazi wenzake kwa ujio wetu.
4. Kupokea wageni wa barmedas.tv waingiao Jiji la Mwanza na waondokao kupitia Uwanja wetu huu mzuri  mkubwa  na wakupendeza.

Kweli tulitembelea Screen Tv zetu tulizoweka hapo Kiwanjani zikitoa huduma kwa ajili ya matangazo na taarifa zingine, ukweli tulifarijika kukuta na kuona kila kitu tulichokusudia kukuta kilikuwa sawa na Wasafiri walikuwa wakisubiri usafiri lakini karibu wote walikuwa wakiangalia Channel mbali mbali za barmedas pasipo kusahau Channel ya MTG iliyokuwa ikitoa taarifa kuhusu ratiba za safari kama picha zinavyoonekana hapo chini.

Ukweli kama tunavyosema MTG inatazamwa na Watu wengi kutokana na taarifa zake  Mahsusi za kibiashara , Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa hivyo endelea kutuunga mkono kujiunga na huduma zetu  pia , kuangalia CHANNEL YA MTG (Mwanza Tv Guide)
'Sisi tunatangulia na wengine, wanafuata".




Comments