JENGO LAPOROMOKA MWANZA-barmedas.tv

JENGO LAPOROMOKA- MWANZA.
Mji wa Mwanza jana ulipata musukosuko na taharuki baada ya vumbi la kifusi na kishindo Stanbic katikati ya Jiji la Mwanza.
kilichosikika majira ya saa 5:18 Asubuhi, kufuatia kuanguka kwa ukuta wa Jengo lilokuwa likiendelea na ujenzi katika Barabara ya Nyerere mkabala  na Bank ya

Kwa mujibu wa majeruhi na mashuhuda wa ajali hiyo, ukuta huo uliporomoka  kutokana uchimbaji wa mashimo ya msingi wa Jengo hilo linalo milikiwa na Kampuni ya Mongo Hardware ya Jijini Mwanza .

Ukuta huo uliporomoka na kusababisha idadi ya majeruhi 7 na  2 kuwa katika hali mahututi ambao wamelazwa katika Hospital ya Rufaa ya Bugando, 

Akiongea na waandishi wa Habari Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Ndugu Baraka Konisaga alisema, ujenzi wa Jengo hilo lililokuwa likijengwa na Kampuni ya Exactlline Engineering  umesimamishwa mara moja mpaka hapo wataalamu wa Majengo watakapo toa ripoti ya kitaalamu kuhusu ujenzi wa Jengo hilo.

Baadhi ya waokoaji wakiendelea na shughuli za uokozi.

Wakazi wa Jiji la Mwanza wakiangalia  Mabaki ya ukuta ulioporomoka.


Baadhi ya majeruhi wakiongea na waandishi wa Habari  katika Hospitali ya Rufaa Bugando.

Comments