24/7 SPORTS CHANNEL- brmedas.t

Kwetu sisi watoto wadogo tunawaendeleza vipaji vyao kila mmoja kumtambua anapendelea nini , nasi huchukua hatua kumwendeleza huyo kijana kama picha inavyoonesha, tumekuwa tukitoa michango mingi katika Jamii kuhakikisha michezo inapewa kipaumbele na tunaitoa hatua moja kuipeleka hatua nyingine.

Tumekuwa na Mikataba ya Miaka 5 kufadhili  Wilaya 2 kwa ajili ya Ligi Daraja la 4 Vyama vya Wilaya tulivyoingia navyo Mikataba ni Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Nyamagana  NDFA na  Chama Cha  Mpira wa Miguu  Wilaya ya Ilemela  IDFA, tumekuwa tukiifadhili michezo hiyo 1, kuhakikisha michezo hiyo inaanza kwa wakati na kuchezwa  mechi zote pasipo mawaa  2. Kuhakikisha michezo hiyo inarushwa LIVE katika Channel yetu ya Michezo 24/7 Sports michezo 700x 2= 1,400  Michezo ambayo tunairusha LIVE na kuangaliwa na watazamaji walioko Dar Arusha Mwanza na Kwenye ONLINE kwani michezo inapo chezwa Channel hii huiunganisha kwenye Channel  Mama ya barmedas.tv na michezo hiyo kuonekana moja kwa moja hii imewafanya wachezaji kujiona wanafanya kitu  cha kuthaminika na huongeza bidii kubwa katika kucheza.

Barmedas.com  hutoa zawadi mara baada ya Ligi kuisha kwa pande zote 2 na hii huhamasisha na kufanya kila mchezaji kujituma katika uchezaji ili kufanikisha adhima yake ya kuwania zawadi, kama Golikipa Bora, Mchezaji Bora , Mfungaji Bora  , Mchezaji mwenye nidhamu, na hata mwamuzi Bora pia  huweza kupata zawadi.





Comments