FRIEND MATCH- barmedas.tv

Barmedas SPORTS CLUB YAPATA MBABE WAKE.

Timu ya  Barmedas Sports Club  jana  ilikutana na kichapo kutoka   timu hatari  ya  HalfLondon  yenye makao yake makuu  Magomeni Kirumba,   kwa kuifunga mabao 2 -1   katika Uwanja wa Magomeni , upande wa HalfLondon magoli  yalifungwa na Kafung Temi Kotecha goli hili lilipatikana katika kipindi cha kwanza na dakika 10 baada ya goli hilo kufungwa mshambuliaji machachari  wa Barmedas  Anzurun Issa alirejesha matumaini na nderemo upande wa timu yake alipoachia mchomo mkali uliomuacha Golikipa akigaa gaa , na hivyo kuisawazishia  timu yake goli   hadi mapumuziko matokeo yalikuwa 1-1.
Kipindi cha pili timu zote ziliingia na hamasa kubwa na kama washambuliaji mahiri Anzurun Issa na Jackson Musa walioonekana kuisumbua sana ngome ya wapinzani wangekuwa makini  wangeibuka na ushindi baada ya kukosa  magoli ya wazi kabisa walipokaribia langoni mwa timu pinzani  aidha  walipiga juu ama kumlenga Golikipa wa timu hiyo  aliyeidaka mipira hiyo kiurahisi .
Goli la 2 lilifungwa na Ismael Matupn na  kuipatia timu yake Goli la ushindi  hivyo hadi kipyenga kinapulizwa kuashilia kuisha  kwa  mchezo huo Barmedas Sports Club 1  HalfLondon 2.
Picha chini waliovalia Jezzy nyekundu Bukuta na T-shirt nyeupe ni timu ya Barmedas Sports Club na walio vaa Nguo za Blue ni HalfLondon , wakiwa katika uwanja wa Magomeni baada ya timu hizi kupata fursa  kucheza mchezo wa Kirafiki.

Comments