BVR-barmedas.tv



Kazi kubwa Serkali imefanya ya kuandaa Daftari la kudumu la wapiga kura, zoezi lililoanza likiwa na changa moto kubwa lililopelekea vyama vya upinzani kuinyoshea mkono  Serkali kuwa zoezi halitafanikiwa kwani halikuwa na maandalizi mazuri ni kama Serkali ilikurupuka kulifanya pasipomaandalizi.

Serkali ilijitahidi kuboresha changa moto zilizokuwa zinapigiwa kelele na vyama kuhusu vifaa kuwa duni vya uandikishaji na hatimae Serkali ilijipanga vyema na kuhakikisha zoezi linafanyika kwa weredi mkubwa hatimae , linaelekea kukamilika baada ya siku 4 zilizoongezwa za kukamilisha katika Mkoa wa Dar - es -Salaam.

Kunahaja ya kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa na moyo wa kutokukata tamaa mapema hata kama jambo alilolianza akiwa na uhakika ya kulifanya na kweli alilipigania na hatimae kulikamilisha salaama ukiachilia mbali vijembe na maneno yanayotolewa ya kubeza juhudi zinazofanywa  na Serkali  chini ya  Uongozi wa Rais Jakaya.

Sasa karibu kila Raia mwema wa Tanzania  aliyekuwa kafikisha umri wa kupiga Kura amepata Kadi yake na sasa yuko tayari kupiga kura wakati utakapo wadia ambao nao si mbali bali ni tarehe 25 Mwezi wa Kumi Mwaka huu  2015.

Image result for kura ya maoni yaahirishwa

Comments