WIMBO WA TAIFA-barmedas.tv

Wimbo wa Taifa lolote unapopigwa Watu wote hushauriwa kuwa na heshima ikiwa ni pamoja na kusimama na kukakamaa mwili kuonyesha heshima  na adabu katika kulipenda Taifa lako wengine hushiriki kweka mikono yao kifuani hiyo hunyesha na kuashilia kuupa heshima wimbi huo wa Taifa.

Kumetokea na tatizo hivi karibuni Vijana wengi sasa wanakuwa hawajui kabisa maana ya Wimbo wa Taifa utakuta haswa majira  wimbo wa Taifa unapopigwa huwa vijana wanaongea, wamekaa ama wanafanya mambo yao tofauti na  kujali  kufuatilia kinachojili mda huo.

Uzalendo umeanza kupungua kutokana na matabaka baadhi wanajiona ndio bora na wengine wanajiona ni wanyonge katika Nchi hii, sababu nyingine kukosekana  kwa Elimu ya Uraia na Maadili nayo ni changamoto kufanya Watu kupungua  kuipenda na kulithamini Taifa lao.

Picha hapo chini inaonyesha viongozi wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kuonyesha upendo mkubwa katika Nchi yao na baadhi wanaonyesha kuweka mikono yao katika kifua na pia wakiwa wanauimba wimbo huo wa Taifa.

Taifa sasa lifundishwe Elimu ya uraia ili kurejesha uthamani Watu kulipenda na kulifilia Taifa lake, tofauti na zamani Watu waliweza kupoteza maisha yao kwa kupigania Taifa liwe na haki,  ndipo tuna waona akina Mkwawa na wengine walipiganana na maadui waliotaka kutwaa haki na mali ya Taifa hili walinyongwa na Wakoloni na kufa lakini kifo chao cha kizalendo leo Nchi yetu ya Tanzania iko Huru.


Comments