RAIS AJAE-barmedas.tv

Rais ajaye, watu wengi wanategemea kabisa kuwa Rais ajaye atakuja kukamilisha na kumalizs kabisa mahitaji na  kero inayomtatiza Mtanzania.

Mimi sidhani Rais ajaye anaweza kumaliza kabisa matatizo na kero zinazo lalamikiwa hilo nisawa .

Watanzania inabidi wabadirike tofauti na sasa vijana wanapiga kelele hawana ajira lakini ukiangalia kabisa vijana wamekuwa wanarundikana na kupiga soga  na kubishana kuhusu siasa hata wakati mwingine kupigana  tendo hilo linafanyika kuanzia Asubuhi hadi jioni , hilo sidhani linawezeka kuleta mabadiriko hata aje Rais wa namna gani.

Vijana wamekuwa wavivu sana lakini  pia hawapendi kutumika hawajitambui  , hivyo mda unakuwa unachomeka  bure , wataendelea kulalamika  na kuilaumu Serkali pasipo yeye Kijana kujitambua na kujua wajibu wake.

Awamu inayokuja kila Rais anajaribu  kueleza jinsi atakavyo kuja kutengeneza Serkali yake lakini pasipo kuandaa mazingira mazuri ili nguvu kazi hii itumike hakika hakuna jipya.

Vijana wamekuwa na tamaa sana kuangalia mwenzake  anafanikiwa nae anapata tamaa pasipokujua mwenzake huenda kajipatia mali hiyo kwa bidii zake lakini upande mwingine huyo kijana kapata mali huenda kwa kuiba sasa vijana inabidi wabadiriki kwani hao ndio nguvu kazi ya kuweza kulipeleka  Taifa kule tunako tarajia.

Elimu yetu sisi tunaidharau na kuona Mtu asipozungumza Kiingreza hana Elimu pasipo kujua kuwa Lugha yetu ya Kiswahili inasoko sana Mataifa mbali mbali wanapenda kujifunza na kuijua Lugha hii bara bara, ukienda kwenye  makolegi sasa wahadhili wa Lugha hii utakuta ni watu kutoka Kenya, Uganda , Rwanda na hata Burundi Watanzania wenye Lugha yao ah wanakuwa wanaichezea tu kipindi cha Mwl Nyerere alipenda kuiendeleza na kuienzi Lugha hii ya Kiswahili

Swala la kuvifufua Viwanda ni lamuhimu sana kwani Viwanda vyote vijianza kufanya kazi Ajira itapatikana na Vijana wataajiliwa na kujipatia maendeleo, Swali langu je hawa Vijana waliozoea kuweka magenge na kuwa Wazembe  Serkali Rais atakuja kuliweka vipi swala hili la Vijana pia kupoteza Maadili ya Kitanzania?

Watu wanakwenda kusikiliza sera za kila Chama na Wagombea Urais wanajinadi pia sisi tujitahidi kusikiliza Sera hizo kwa makini jaribu kuwachambua kwa maneno yao na utapata jibu ili siku ya kura ijue nani atakuletea maendeleo.

Watu wanafurika kwenye Mikutano ya Kampeni lakini je wote wanakwenda kuwasikiliza vyema wagombea Uraisi, Ubunge na Udiwani wanakuwa na utambuzi kwa yale yasemwayo ama wanakwenda kwa Ushabiki tu na hawatakuwa na maamuzi kwa maana hata kura kuipiga hawatakuwa na haki labda  hawajajiandikisha  ili wapige kura.

Tunapokwenda kupiga kura siku zinaenda kuyoyoma inatubidi Wapiga kura makini sana katika kumuchagua Rais ambaye wengine wanasema awe maili sana, mimi nasema Rais ajaye awe ni mbunifu na ajue kupanga kete namuna yakuwatumikia Watu wote pasipo ubaguzi na kulijenga Taifa kuwa moja na kuondoa nyufa ambazo sasa zipo zinaendelea kujitokeza.

Tanzania itasimama na kulifanya Taifa kuwa wamoja kama Waasisi wetu walalivyolijenga taifa lenye umoja na nguvu.

Watanzania sasa waendrlee kumuomba Mungu ili Taifa letu livuke kwa Amani kipindi hiki ili tuendelee kuwa na Amani tele.

Mungu Bariki Tanzania ,Mungu Bariki Afrika.


Comments