Barmedas SPORTS CLUB- barmedas.tv

Kikosi kamili cha Barmedas.Sports Club enzi zile kikiwa kinaongozwa Mchezaji wa Kimataifa 8 na pia ndiye Mkurugenzi wa Barmedas.Comwakipiga picha ya pamoja na kikosi kizima cha Barmedas Sports Club mara baada ya timu hiyo kuzichachafya timu nyingi walizokutana nazo na Majuzi kuikung'uta timu kali ya UHAMIAJI YA WILAYA YA NYAMAGANA timu hizi zilipokutana ana kwa ana Mwezi jana.
Timu ya Barmedas Sports Club imejiwekea malengo kuwa na Michezo 2 kila Mwezi na hii pia inawafanya wafanyakazi kuwa na Afya njema kwa kujijenga afya zao kwa kupitia Michezo iliyopo katika Kampuni hii.
Alipoulizwa swali captain wa timu hiyo Anzurun Issa kwamba mbona wanacheza na timu changa kwa nini wasijitupe kucheza na timu kubwa alikuwa mkali katika kujibu swali hilo " Timu gani ni ndogo timu tulizocheza nazo zote ni kubwa na zinawachezaji wakiwango cha juu hivyo sema timu yetu tuna jipanga vyema"
Akijibu swali la kuwa wanapata mda upi wa kufanya mazoezi ! Captain huyo mwenye maneno ya kujitapa " huwa tunatenga mda kwa week tunafanya zoezi japo mara moja lakini pia wachezaji wetu hufanya mazoezi katika timu zao za Mitaani ambapo wamo wachezaji wanacheza kwenye timu za Daraja la 3" akitakiwa ahakikishe Wachezaji hao ni wapi? hakusita kujitaja mwenyewe kwanza Anzuruni issa, Eli'ejah Sokoro,Jackson Musa, Charles -akiwa ni Golikipa, Juma juma , alipoambiwa aendeleea kuwataja wachezaji anaosema ni Mahiri alitaja jina la Mkurugenzi wake Mohin ambaye ni mchezaji wa kimataifa , alipoulizwa mbona kuna Match 2 zimepita hajaonekana Captain huyo alijibu kwa ukali kuwa , Mkurugenzi anamambo mengi anapata mda nadra sana kucheza mfano kwa sasa yuko safari nje ya Nchi kikazi"





Comments