MWENGE WA UHURU-barmedas.tv

Mwenge wa uhuru unaokimbizwa sasa Tanzania nzima,  uliwashwa kwa nadhumuni yakuleta mshikamano na Umoja  pia  matumaini kwa Mtanzania.
Mwenge huu tangia uanze kukimbizwa umeonyesha shughuli nyingi hufanywa kipindi hicho kila unapopita Miradi mingi hufunguliwa tena yenye thamani kubwa na pia hufufua shughuli ambazo zinakuwa zimezorota.
Hivi sasa Mwenge unapita kila Mkoa , Wilaya, Tarafa na vitongoji hupita ikiwa na Kauli mbiu na hivyo viongozi wa sehemu husika huhakikisha ratiba yote ilivyopangwa inatekelezeka na Mwenge unakimbizwa sehemu hiyo kwa usalama na Amani tele.
Tangia kipindi cha Mwalimu Nyerere Mwenge umekuwa ukikimbizwa kila Mwaka na kupita kila sehemu ukifufua Miradi iliyokufa na kuanzisha Miradi mipya na hivyo kweli Watanzania tangia kipindi hicho wameona Mwenge kama ni alama yenye kuwaunganisha Watanzania pia kuleta matumaini katika Nchi yao.
"Sisi tunawasha Mwenge na kuuweka katika Mlima Kilimanjaro ili kumulika Mipaka yetu na kuleta matumaini" hiyo ilikuwa kauli ya Mwalimu Nyerere na viongozi wenzake walipoyatamka haya walikuwa na shauku kubwa kuhakikisha Tanzania inakuwa salama na kuleta matumaini kati ya Mtu na Mtu mda wote.
Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu utakao fanyika Mwezi October 2015 kwa kuwa chagua Madiwani , Wabunge na Rais hapa tunahitaji upendo na Amani ili kulifikisha zoezi hili kwa Amani , mshikamano  , Upendo na utulivu ili Nchi yetu iendelee kuwa na Amani na Umoja .
Mwenge ni alama inayoleta  Umoja matumaini na kuondoa   umasikini na ujinga  pia kumulika ili Mtanzania  apate kuifurahia Nchi yake na kula matunda ya ya Tanzania.

Comments