EDWARD NGOYAI LOWASA-barmedas.tv





Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Ngoyai Lowassa.
HAKUNA adui wala rafiki wa kudumu katika siasa. Huu ni msemo ulioasisiwa na mwanadiplomasia wa Israel, Avil Primor ambaye amepata kufanya kazi katika nchi mbalimbali duniani, ikiwemo ubalozi wa nchi yake nchini Ujerumani (1993-99) na katika Umoja wa Ulaya (1987-91).

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumzia urafiki kati ya nchi yake na Iran ulivyokuwa. Kabla ya mapinduzi ya nchi hiyo ya Kiarabu ambayo ni taifa la Kiislamu mwaka 1979 yaliyomuweka katika himaya Ayatollah Khomeini, wawili hao walikuwa ni marafiki wa kufa mtu. Enzi hizo, Iran ilikuwa ni ardhi pekee kati ya mataifa yote ya Kiarabu, ambayo yaliruhusu ndege za Israel kutua!

Leo, unapoitaja Iran mbele ya Israel ni sawa na uhai na kifo. Ni maadui ambao kila mmoja anatamani mwenzake ateketee mara moja. Lakini Primor, licha ya kusema hakuna adui wala rafiki wa kudumu katika siasa, aliongeza kuwa kilicho cha kudumu kwa wanasiasa ni masilahi yao!

Hilo ndilo tunalolishuhudia leo baada ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Ngoyai Lowassa anapokuwa sehemu ya jeshi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambacho kwa miaka mingi, kimemtaja kama mmoja wa mafisadi wanaostahili kuogopwa katika nchi hii.

Mwaka mmoja kabla hajajiuzulu kwa kashfa ya kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond, Lowassa alikuwa mmoja wa viongozi 11 waliotajwa na Dk. Willbroad Slaa kuwemo katika orodha ya mafisadi iliyojipatia umaarufu kama List of Shame.

Katika orodha ya watu hao waliotajwa, wapo wengine ambao pia wamehusishwa katika kashfa nyingine zilizohusu uporaji wa mabilioni ya shilingi za umma kwa kutumia nafasi zao za kiuongozi walizopata kuzishikilia siku za nyuma au hadi sasa wakiwa katika ofisi za umma.

Akiwa serikalini, tangu enzi za Rais William Mkapa na sasa Jakaya Kikwete, Lowassa alikuwa mmoja wa viongozi wa juu waliokuwa wakitoa maneno mengi ya kejeli, kashfa na dharau kwa vyama vya upinzani vilipojaribu kwa namna yoyote, kuhatarisha neema za wakubwa wa chama na serikali.

Na Chadema, kimejipatia umaarufu mkubwa kwa jamii ya wanyonge baada ya kuonesha kuwa ni chama chenye nia ya kupambana na ufisadi na kutowajibika kwa viongozi wa umma, kiasi kwamba idadi kubwa ya wafuasi wake ni watu waliokata tamaa na ambao kwa namna moja au nyingine, hawafaidiki moja kwa moja na uwepo wa CCM madarakani.

Hivyo Lowasa kuhama kutoka katika Chama tawala na kwenda Chama cha upinzani hii inaonyesha ni jinsi gani Lowasa anavyohitaji kuhakikisha anakuwa Rais wa Tanzania kwa kukikalia kiti kikubwa kuliko vyote katika mfumo uliopo Tanzana.

Moja kwa moja siwezi kueleza kuwa Lowasa alikuwa na ndoto ya kukihama Chama chake haswa katika  siku chache na ghafla kiasi hiki lakini baada ya kuenguliwa jina lake ( kukatwa)  hapo alianza kutafuta njia mbadala tena inaonyesha kwa hasira na machungu makubwa na hii akionyesha safari yake ya Matumaini inaweza nyoka ikawakia huko UKAWA, na sasa anajipanga kuwania nafasi hiyo baada ya viongozi wa UKAWA kumpokea kwa mikono miwili.

Kwa sasa kila mmoja anachuchumia kuona anajipatia ushindi kati ya QWashindani hawa wawili wakubwa kati ya John Pombe Magufuli  na Edward Ngoyai  Lowasa ndio majina yanayoonekana sasa kutajwa na wapiga kura kuwa mmoja wapo akizicheza Karata yake vyema,  kama navyorudia kukukumbusha wewe msomaji kuwa Siasa ni Sayansi yenye mbinu na Hesabu kali kuweza kujikuta unamshinda mpinzani wako, hivyo wacha tuone mwisho wa mchezo huo unaishia wapi Mwezi Octoba  2015.


Comments