LOWASA ABADILI UPEPO-barmedas.tv

Siku ya tatu baada ya kutangaza rasmi kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema akitokea Chama cha Mapinduzi CCM, aliekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Monduli Edward Ngoyai Lowasa, leo amechukua Fomu ya Kugombea Urais.

Mamia ya Wananchi , pamoja na makada wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA, yamejitokeza katika kumsindikiza Lowasa wakati wa zoezi la Uchukuaji wa Fomu lililofanyika Makao Makuu ya Chadema Jijini Dar es salaam.
Lowasa amechukua fomu huku viongozi waliodaiwa kutokubaliana na maamuzi ya yeye kupokelewa chadema wakiwepo ambao ni pamoja na Katibu Mkuu Dk.Wilbroad Slaa, Naibu Katibu Mkuu Bara John Mnyika pamoja na Mwanasheria Mkuu Tundu Lisu.
Duru za kisiasa kutoka ndani ya vyama vinavyounda Ukawa zinaeleza kuwa Lowasa anatarajia kuwa mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu unaotarajia kufanyika Octoba 25 akiwakilisha Vyama vinavyounda Ukawa.
Hata kabla ya kampeni za wagombea kuanza rasmi, mchuano umeonekana kuwa mkali katika vijiwe mbalimbali na hata katika mitandao ya kijamii ambapo mijadala mikali ni kati ya Lowasa na Mgombea wa CCM Dkt.John Pombe Magufuli.

Hivyo uchaguzi wa Mwaka huu 2015 hapo October utakuwa ni mkali sana na kila upande unajaribu kuzicheza Karata vyema maana siasa na Sayansi na pia Hesabu.
Isipokuwa uchaguzi wa Mwaka umekuwa  namtindo mwingine baada ya wana siasa kwenda vyama vingine  kuchukua nafasi kwa ajili ya kugombea nafasi na hii imevichanganya vyama husika baada ya wenyeji kuona wageni wanaingia na kuwania nafasi, na hii imeanza kuvimega vyema na kuleta makundi baada ya upande mmoja kuona faraja wageni kuleta neema lakini  baadhi ya wenyeji hawafurahishi kuona wageni wanakuja kuzivuruga harakati na msukomo waliokuwa wamejipanga kuingiliwa na wageni.

Comments