CELINA KOMBANI-barmedas.tv

TAIFA LIMEFIKWA NA MSIBA MKUBWA.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani amefariki Dunia jana jioni Tarehe 24 Sept 2015 ,  katika Hospitali ya Appolo nchini India, alikokwenda kupata matibabu.
Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashillilah alisema Kombani alipelekwa nchini humo wiki tatu zilizopita.“Ni Kweli amefariki dunia leo jioni (jana) ndiyo ninachoweza kusema kwa sasa,” alisema Dk Kashillilah kwa ujumbe mfupi bila kueleza waziri huyo alikuwa akisumbuliwa na nini. Katika mchakato wa kura ya maoni ndani ya CCM, chama hicho kilimpitisha Kombani kuwa mgombea tena ubunge katika jimbo la Ulanga na alikuwa kafanya vizuri katika mchakato mzima.
Waziri huyo alishiriki vikao vyote vya Bunge la Bajeti lililomalizika mwezi juzi mwaka huu, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2015/16.
Wasifu wa Celina KombaniCelina Kombani alizaliwa Juni 19, 1959.Alisoma katika Shule ya Msingi Kwiro mwaka 1968-1975, Sekondari ya Kilakala 1975-1978 na baadaye katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Tabora kwa masomo ya juu 1979-1981.Baada ya masomo ya elimu ya sekondari.
Kwa mjibu wa utaratibu ni kuwa endapo mgombea atafikwa na mauti Chama hicho kitafanya uchaguzi kujaza nafasi iliyoachwa wazi ndivyo itakavyokuwa kwa Chama cha Mapinduzi kuteua mgombeaji mwingine ambaye ataziba pengo la Marehemu Celina Kombanim
Mama huyo kwa njibu ya hata wakazi qaeneo hilo alilokuwa akikiwakilisha wamepatwa na mushituko mkubwa kusikia habari za kifo cha Celina Kombani na anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatatu kama taratibu zitajuwa zikiendelea kama zilivyoratibiwa.
Katika kipindi hiki cha majonzi tunaiombea Familia  moyo wa subira ili Mungu awe katikati ya familia ndugu na jamaa wote na hata Taifa zima kutokwa na mchapa kazi na pia muzoefu katika utumishi kitaifa,  ambapo taifa lilikuwa bado likimuhitaji fikira zake na busara zake pia.
Bwana alitoa , na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe daima na hata milele, Amen.

Comments

Popular Posts