BARAZA LA MADIWANI-barmedas.tv

Mwanza   
Baraza la madiwani  halmashauri ya jiji la Mwanza limepitisha bajeti ya kiasi cha shilingi billion 87. 194 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ikiwa ni ongezeko la asilimia 52 ya bajeti ya mwaka ulipo 2015/2016
Mwaka wa fedha unaoendelea hadi sasa 2015/2016 halmashauri ya jiji la Mwanza ilikuwa na bajeti ya shilingi billion 57.307 ambapo hadi kufikia mwezi December mwaka 2015 halmashauri imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi billion 28.357 sawa na asilimia 49.

Kupitia bajeti hii mpya halmashauri itaongeza mapato yake kwa asilimia 62 kutoka shilingi bilioni 11.409 mwaka uliopo hadi shillingi bilioni 15.061 kwa mpya .
Akiwasilisha Bajeti hiyo katika kikao maalumu cha baraza hilo kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya jiji la Mwanza kikiongozwa na mstahiki meya wa jiji la Mwanza bwana James Bwire, mchumi wa jiji Joseph Kashushura amesema  katika bajeti ya mwaka huu asilimia 60 ya bajeti itapelekwa kwenye miradi ya maendeleo
Mbunge Nyamagana  bwn. Stanislaus Mabula amesisitiza kuipa kipaumbele miradi ambayo ilianza kutekelezwa katika bajeti iliyopo na haijakamilika ili kuikamilisha kupitia bajeti mpya ya mwaka 2016/2017.

Aidha madiwani wametumia fursa hiyo kumpongeza mkurugenzi wa jiji bwana Adam Mgoyi  na Mbunge wa Nyamagana kwa kazi kubwa za maendeleo za jiji walizozifanya mwaka wa bajeti ambao unaelekea ukingoni.






Comments